Friday, 6 April 2018

Majibu Nabii Tito mgonjwa wa akili au la kujulikana Aprili 13HAKIMU mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Dodoma, James Karayemaha amesema amepokea taarifa za vipimo vya kitabibu dhidi ya Tito Machibya maarufu kama Nabii Tito.

Vipimo hivyo ni vile ambavyo mahakama iliagiza mtuhumiwa huyo apimwe ili kubaini iwapo anakabiliwa na tatizo la afya ya akili au laa. Amesema ataipitia ripoti hiyo na kuitolea uamuzi hapo Aprili 13 mwaka huu.


Nabii Tito

“Nimepokea taarifa ya kitabibu kuhusu mtuhumiwa leo asubuhi, hivyo nitaipitia ripoti hii, Aprili 13, 2018 nitaitolea uamuzi,” amebainisha Karayemaha.

Hata hivyo, wakati hakimu akitoa maelezo hayo, mtuhumiwa huyo hakufikishwa mahakamani. 

Hatua ya mahakama kuamuru mtuhumiwa huyo anayekabiliwa na tuhuma za kutaka kujiua apimwe akili ilikuja baada ya yeye mwenyewe kudai mahakamani hapo kuwa ana matatizo ya akili yaliyosababisha afanye jaribio hilo.

Mtuhumiwa huyo yupo mahabusi hadi Aprili 13, mwaka huu ambapo hatma ya kesi hiyo itajulikana.

No comments:

Post a Comment