Monday, 9 April 2018

Mamis waajiriwe shirika la ndege la Taifa – Mwakyembe
Peter Simon

WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amependekeza kuwa wanaoshiriki mashindano ya urembo wa ma-miss waajiriwe katika shirika la ndege la taifa kwa sababu wana vigezo vya kutosha.

Dk. Mwakyembe alitoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo kwa mwaka 2018 yatakayofanyika chini ya kampuni ya The Look baada ya ile ya Lino kuachia ngazi hiyo.

Amesema washiriki wengi wa mashindano hayo wanakuwa na uwezo na sifa nyingi za kuwa katika cabin crew ila tu kabla ya kuajiriwa wanapaswa kupelekwa kupatiwa mafunzo mafupi kwa wa miezi mitatu katika chuo cha anga kabla ya kuanza kazi na hii itapunguza tatizo la ajira kwa warembo hao.

“Hii pia inaweza kusaidia baadhi ya wasichana kwa sababu kuna warembo wamekuwa wakishiriki mashindano hayo na baadaye dira zao za maisha kupotea na kujikuta wakiishi maisha magumu,” amesema.

No comments:

Post a Comment