Saturday, 14 April 2018

Marekani, Ufaransa na Uingereza zashambulia Syria Syria


Shabulio Syria
MATAIFA ya Marekani ,Ufaransa na Uingereza yamefanya mashambulio yakilenga vituo vitatu huko Syria kama adhabu kwa madai kwamba utawala wa Rais Bashar al Saad, ulitumia silaha za kemikali dhidi ya raia wake.
Taarifa zinasema milio ya milipuko imesikika katika maeneo kadhaa ya miji ya Damascus na Homs.
Katika taarifa yake Rais Trump amedai kwamba vituo vilivyo lengwa vinahusiana na utafatiti wa uhifadhi na utengenezaji wa silaha za kemikali.
Rais Trump ameongeza kusema kwamba Marekani iko tayari kuendeleza mashambulio hayo hadi utawala huo wa Syria utakapokoma kabisa kutumia silaha za kemikali.
Pia ameilaumu Urusi kwa kutomdhibiti mshirika wake kutotumia silaha hizo kama ilivyoahidi 2013.
Kutokana na hatua hiyo, Rais Putin ameshtumu vikali mashambulizi yaliyofanywa dhidi ya Syria - akitaja mashambulio hayo kuwa uchokozi mkubwa.
Hata hivyo, wizara ya ulinzi ya Urusi inasema zana za serikali ya Syria za mfumo wa kujikinga zimefanikiwa kudungua makombora yote kumi na mbili yaliyovilenga vituo vya kijeshi vya huko Damascus ingawa hawakutoa ushahidi wowote.
Helikopta zilizokua katika kituo hicho zinasemekana ndizo zilizotumika kufanya shambulio la kemikali huko ngome ya waasi ya Douma.
Urusi pia imesema vituo vyao vya kijeshi havikuathiriwa na mashambulio yaliofanywa na Marekani ,Ufaransa na Uingereza.
Hata hivyo, vyombo vya habari vya serikali ya Syria vinasema mashambulio hayo kwenye kituo cha utafiti cha Damascus yalisababisha uharibifu mdogo na mashambulizi katika mji wa Homs yalijeruhi .
Ripoti zingine zinaashiria kuwa baadhi ya zana na vifaa vya kijeshi kwenye maeneo hayo vilikuwa tayari vimeondolewa mapema wiki hii kabla ya shambulio hilo.

Chanzo: BBC

No comments:

Post a Comment