Saturday, 14 April 2018

Matatizo ya wanandoa yasiwe sababu ya kumwathiri mtoto – Makonda


Paul Makonda 

Peter Simon

MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema matatizo ya wanandoa hayatakiwi kumuathiri mtoto kiasi cha kumnyima haki zake.

Ameyasema hayo leo Aprili 14, 2018 katika mahojiano maalumu yaliyorushwa mubashara na televisheni ya taifa, TBC.

Amesema hata kama mtoto amezaliwa nje ya ndoa, ana haki sawa na aliyezaliwa ndani ya ndoa, ndiyo maana sheria ya mtoto (ya mwaka 2009) haijasema ni mtoto yupi, bali inamgusa kila mtoto.

“Haijalishi mtoto amezaliwa na ‘house girl, sheria haibagui mtoto inawalinda watoto wote.

“Ajenda kuu tunayoizingatia ni haki ya mtoto. Watoto wote wa ndani na nje ya ndoa wana haki sawa,” amesema.

Kadhalika, amewataka viongozi wa dini kutoa mafunzo ya malezi na wajibu wa wazazi kwa watoto kabla ya kufikia hatua ya kufunga ndoa.

“Mapungufu yaliyopo katika sheria yanawafanya maofisa wa ustawi wa jamii waonekane hawafanyi kazi. Mapungufu haya ya kisheria yanawanyima kufanya kazi kwa ufanisi,” amesisitiza.

No comments:

Post a Comment