Thursday, 19 April 2018

Mazoezi yanatuondoa katika uwezekano wa kukumbwa na kiharusi


Mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai akizungumzia umuhimu wa kufanya mazoezi ya viungo, kupunguza ulaji wa nyama nyekundu na kujenga utamaduni wa kutumia kitunguu swaumu kuepuka maradhi ya kiharusi.


MWANADAMU ni kiumbe ambaye hujipatia riziki zake kutokana na kufanya kazi iwe za kilimo, ofisini au biashara. Bila kufanya kazi mwanadamu hawezi kujipatia riziki labda yule ambaye ni tegemezi kama mtoto au mzee.

Hata hivyo, uwezo wa mtu kufanya kazi kwa ufanisi unategemea afya yake kuwa njema, kinyume na hapo hawezi kushiriki katika kazi zozote za kujiletea maendeleo.

Yapo magonjwa ambayo yakimpata mtu hawezi kushiriki vema kazi za ujenzi wa taifa, ambapo miongoni mwayo ni ugonjwa wa kiharusi.

Ugonjwa huo ambao pia huitwa ugonjwa wa kuvamia ubongo, hutokea wakati ambapo mishipa ya damu ubongoni mwa mtu huziba na kupasuka na kufanya baadhi ya seli za ubongo kufa.

Kwa maana hiyo, mwanadamu akipata tatizo hilo upo uwezekano mkubwa wa kubadilisha maisha yake kwani kipato hupungua na pengine kutoweka kabisa kwa kuwa hawezi kushiriki kazi za aina yoyote ambazo zitampa kipato.

Pia anakuwa katika uwezekano mkubwa wa kupoteza uhai wake hasa atakapopuuza kwenda kupata huduma za utabibu.

Mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai, anasema zipo aina mbili za kiharusi zinazojulikana kama Ischaemia na Haemorrhage.

Anasema aina ya kwanza ya kiharusi Ischaemia hutokana na mshipa uitwao kwa kitaalamu arteri unapoganda damu, hivyo damu hiyo kushindwa kusafiri hadi kwenye ubongo.

Mtaalam huyo anafafanua kuwa hali hiyo inaweza kutokea kwa kusababishwa na kitu kinachoitwa thrombosis, ambapo damu huganda kwenye mshipa mkubwa wa arteri.

Anasema mshipa huo ni muhimu katika mwili wa binadamu kwa kuwa ndiyo unaosafirisha damu kupeleka katika ubongo.

Hali hiyo inaweza pia kusababisha vimirija vidogovidogo vinavyopeleka damu katika ubongo kuziba kitendo ambacho wataalamu wa afya au tiba wanakiita lacunar stroke.

Akizungumzia aina ya pili ya kiharusi haemorrhage, anasema mtu hukumbwa na aina hiyo ya pili baada ya kupasuka mshipa kwenye ubongo na kusababisha damu kuvuja yaani haemorrhage.

Mandai anasema hali hiyo hutokea baada ya damu iliyovuja kukandamiza ubongo hali inayosababisha uhalibifu mkubwa kwenye ubongo kwa kuwa ni kiungo laini sana katika mwili wa binadamu.

"Kitendo cha damu hiyo kuganda katika ubongo licha ya kuharibu eneo hilo katika fuvu la kichwa, lakini pia huharibu chembe hai kwenye ubongo hivyo kuhatarisha maisha ya mgonjwa na hali hiyo inaitwa kitaalamu cerebral au haemorrhage ambayo uvujaji wa damu hufanyika ndani ya ubongo," anaeleza.

Anasema pia mtu anaweza kukumbwa na kiharusi baada ya kupasuka mshipa wa damu ambao unazunguka ubongo.

Mtaalamu huyo anabainisha kwamba kabla ya mtu kupatwa na kiharusi, huonesha dalili fulani, ambazo kama zikigundulika mapema na kushughulikiwa anaweza kunusurika na athari zake.

Anasema mgonjwa anapowahishwa hospitalini ndani ya muda wa saa 3 na kupewa matibabu yanayostahili anaweza kupona kabisa.

"Tunatakiwa tule kwa wingi matunda na mboga za majani kila siku. Pia tunatakiwa kula kwa kiasi kidogo vyakula kama vile nyama nyekundu, vyakula vya kukaanga na tunatakiwa tule kiasi kidogo sana cha sukari bila kusahau kunywa maji mengi kila siku, angalau lita moja," anasema  mtaalam Mandai.

Anaongeza kuwa kushindwa kuzingatia kanuni hizo, ni kukaribisha matatizo mengi ya kiafya, ikiwemo ugonjwa huo hatari ambao unawaondoa watu wa umri wa kutegemewa.

Aidha, Mandai anasema mtu mwenye kiharusi anaweza kutibiwa kwa kitunguu swaumu licha ya kwamba anatilia mkazo watu kujiwekea utaratibu wa kula kitunguu swaumu kama sehemu ya kinga dhidi ya magonjwa mengi.

Anafafanua kuwa punje tisa za kitunguu swaumu kilichomenywa kichanganywe na mafuta ya nazi mililita 200 kisha mchangayiko huo mgonjwa auchue sehemu husika asubuhi, mchana na jioni sanjari na kutafuna punje nyingine tatu kila baada ya tukio hilo.

Mtaalamu huyo anasema tiba nyingine ni udi kala, ambapo mgonjwa anatakiwa autafune kwani unasaidia kufungua mishipa ya fahamu.

Anasema iwapo mgonjwa atatumia bidhaa tajwa na kutojisikia nafuu ni vema akamwona ili apate msaada mwingine zaidi wa tatizo hilo.

Licha ya tiba hiyo, Mandai anasisitiza mgonjwa anatakiwa afanye mazoezi ya viungo kwani yanasaidia kuamsha mishipa ya fahamu iliyolalala.

Hata hivyo, anatilia mkazo jamii kuepuka ulaji wa vyakula vyenye mafuta na sukari nyingi, kwani unaweza kumweka mtu katika mazingira ya kumwepusha na magonjwa ya aina mbalimbali yakiwemo yasiyoambukizwa kama kiharusi, kisukari, shinikizo la damu na saratani.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho vinavyozalishwa na kampuni yetu.


No comments:

Post a Comment