Wednesday, 4 April 2018

Mbunge adai wanaume kuoa wake wengi kunapunguza matatizoMBUNGE Gathoni wa Muchomba kutoka Bunge la Kenya amefufua tena mjadala wa iwapo wanaume wanafaa kuwaoa wanawake wengi.Muchomba ambaye ni mwakilishi wa wanawake kutoka kaunti ya Kiambu, amesema wanaume wakiwaoa wanawake wengi mengi ya matatizo ya kijamii yatafikia kikomo.
Gathoni wa Muchomba

Video yake akitoa mwito kwa watu wa jamii ya Wakikuyu kurejelea utamaduni wa kuwaoa wake wengi imesambaa sana katika mitandao ya kijamii nchini humo.
Amedai tangu jamii hiyo ilipotupilia mbali utamaduni huo, matatizo mengi yametokea ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya watoto wanaorandaranda mitaani.
Mwaka 2014, Rais Uhuru Kenyatta aliidhinisha Sheria ya Ndoa ambayo inawaruhusu wanaume kuoa wanawake wengi kisheria iwapo watasajili ndoa zao kama za kitamaduni au za Kiislamu.
Wakristo hata hivyo hawaruhusiwi kuoa wake wengi chini ya sheria hiyo.
Muchomba amesema wengi wa wabunge tayari wamewaoa wake wengi na “wanajivunia” jambo hilo.

No comments:

Post a Comment