Wednesday, 4 April 2018

Mbunge ahoji ni lini Zanzibar itaruhusiwa uwakilishi EACMBUNGE wa Kojani, Hamad Salim Maalim (CUF), amehoji ni lini Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaruhusu Zanzibar kuwa na uwakilishi rasmi katika Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC).

Katika swali lake bungeni leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu, amesema amefikia hatua ya kuhoji hilo kwa kuwa mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar yanaitambua Zanzibar kuwa ni nchi.

Akijibu swali hilo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Augustino Mahiga amesema Ibara ya pili (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na mabadiliko yake imebainisha eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar. Pia ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo.

“Naomba kulihakikishia bunge kuwa maslahi yote ya Zanzibar katika Jumuia ya Afrika Mashariki yanazingatiwa ipasavyo,” amesema Mahiga.

No comments:

Post a Comment