Tuesday, 24 April 2018

Mchumba mpya wa Zuma alazimishwa kujiuzulu kazi yake


Jacob Zuma
MWANAMKE ambaye anatarajiwa kuwa mke wa saba wa aliyekuwa rais wa Afrika kusini, Jacob Zuma amelazimishwa kujiuzulu ajira yake ya ukuu wa asasi isiyokuwa ya kiserikali na chombo cha habari cha nchini humo.
Nonkanyiso Conco ambaye ana uhusiano wa kimapenzi na Zuma ambaye amemzidi umri wa miaka 52, yuko kwenye asasi inayohamasisha kampeni ya kuwawezesha mabinti wadogo katika maisha yao ya kila siku na kuacha kuwategemea wanaume wenye umri mkubwa.
Conco mwenye miaka 24 amejifungua mtoto wa Zuma katika hospitali binafsi iliyoko mjini Durban.
Zuma mwenye watoto 20 sasa, ana umri wa miaka 76,ana wake wanne na mwingine mmoja waliachana na mke wa sita alijiua mwaka 2000.
Conco analazimika kujiuzulu cheo chake akiwa ni ofisa mawasiliano wa kampeni ya kukabaliana na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa wanawake wadogo, unyanyasaji wa kijinsia na ujauzito kwa watoto wadogo.
Hadi sasa Conso hajazungumza chochote kuhusu tuhuma zinazomkabili lakini amewasilisha barua ya kujiuzulu kazi katika shirika analofanyika kazi, Daily Maverick limeripoti.
Habari za uhusiano baina ya Jacob Zuma na Nonkanyiso Conco zilizagaa sana tangu siku ya Ijumaa iliyopita.
Nonkanyiso Conco
Chanzo; BBC

No comments:

Post a Comment