Thursday, 12 April 2018

Mchungaji Msingwa akana kuzaa nje ya ndoa


Mchengaji Peter Msingwa


MBUNGE wa Iringa mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema), ameendelea kukana madai ya kumtelekeza mtoto na kueleza kuwa taarifa hizo zinaenezwa na Jerry Muro.

Akizungumza na EATV, Mchungaji Msigwa amesema madai hayo hayana ukweli wowote na kueleza iwapo lisemwalo lipo basi mhusika amtafute katika namba aliyoitoa na ikishindikana amfuate bungeni.

“Mimi nitamtambuaje huyo mtoto, hiyo picha wameweka tu, ilipoanzia ni kwa Jerry Muro ndio ameanza kusambaza hizo habari kwamba mimi nina mwanamke aliyeenda kwa Makonda amejieleza ndio nimemuacha.

“Ninachokijibu pale, nakijibu kitu ambacho ameanzisha Jerry Muro, kwamba kuna mtu nimemtelekeza amekuwa akinitafauta na nimekuwa nikimzuia, nimejibu kwamba kama mtu huyo yupo nimekuwa nikitoa namba zangu za simu na kama sipatikani aje hapa bungeni,” amesisitiza.

Kuanzia mwanzoni mwa wiki hii mamia ya wanawake wamejitokeza ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ili kupata msaada wa kisheria baada ya kutelekezwa na wazazi wenzao. Pia RC Makonda ametoa nafasi ya kuwasikiliza wanaume waliotelekezwa na wake zao ambapo watapatiwa msaada wa kisheria pia.

No comments:

Post a Comment