Wednesday, 25 April 2018

Mdee ahoji bilioni 495/- za ATCL


Halima Mdee

MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) ameikosoa serikali baada ya kutenga sh. bilioni 495 bilioni kununulia ndege mbili.

Wakati akichangia katika mjadala wa bajeti ya Wizaya ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka 2018/19 jana Bungeni, Mdee amesema hata taarifa za Msajili wa Hazina mwaka 2015/16, zinaeleza wazi kuwa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) halina mpango wa biashara wala wataalamu.

“Hoja si kupinga ununuzi wa ndege, hoja ni fedha hizi za ununuzi wa ndege zitazalisha au tunazipoteza. Taarifa ya ATCL inaeleza wazi kuwa haikuwa na mpango wa biashara. Yaani tunawekeza fedha katika shirika ambalo halina mpango wa biashara.

“Shirika lina madeni lakini tunanunua ndege hizi. Bunge litekeleze wajibu wake. Hivi kilimo kinachoajiri Watanzania wengi tunakiwekea fedha kidogo lakini kwenye ndege ambazo tunajua tunakwenda kumwaga fedha chini tunawekeza sh. trilioni 1.” amesisitiza.

Katika bajeti, ATCL imetengewa sh. bilioni 495 kununua ndege mbili; moja aina ya Q400 yenye uwezo wa kubeba abiria 76 na nyingine kubwa ya masafa marefu aina ya Boeing 787-8 (Dreamliner), yenye uwezo wa kubeba abiria 262.

No comments:

Post a Comment