Thursday, 19 April 2018

Mke wa rais msaafu wa Marekani George HW Bush aaga dunia

Barbara Bushi wakati wa uhai wake

MKE wa rais wa zamani wa Marekani na mwanaharakati, Barbara Bush, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 92.
Barbara, ndiye aliyekuwa nguzo ya kisiasa ya marais wawili wa taifa hilo akiwemo mumewe George HW Bush na mwanawe George W Bush.
Mama huyo ambaye alikuwa mke wa rais kutoka 1989 hadi 1993 amekuwa akidorora kiafya kwa muda sasa na alikuwa amekataa kupatiwa matibabu zaidi.
Risala za rambirambi zimetumwa nchini Marekani kutoka maeneo tofauti duniani.
Mumewe aliye na umri wa miaka 93 ndiye rais aliyeishi kwa muda mrefu nchini Marekani.
Mwana wao George alichaguliwa 2000 na kuhudumu kwa mihula miwili kama rais wa 43 wa Marekani.
Katika tanzia amesema katika taarifa yake kwamba ''mamangu mpendwa ametuacha akiwa na umri wa miaka 92. Laura, Barbara, Jenna na mimi tunaomboleza, lakini roho zetu zimepumzika kwa sababu tunajua yake pia imepumzika.

No comments:

Post a Comment