Wednesday, 18 April 2018

Mkurugenzi CIA alifanya ziara ya kisiri Pyongyang
                              Mike Pompeo                           MKURUGENZI wa Shirika la Upelelezi la Marekani(CIA),Mike Pompeo alisafiri hadi mjini Pyongyang kwa mkutano wa kisiri na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un , kulingana na vyombo vya habari vya nchi hiyo.
Mkutano huo ulioandaliwa kuandaa mkutano mwingine kati ya rais Donald 
Trump na Kim Jong Un, ulifanyika wikendi ya sikukuu ya Pasaka , kulingana na maofisa ambao hawakutajwa.
Rais Trump amekiri kufanyika mazungumzo ya hadhi ya juu na Pyongayng. Lakini mkutano huo wa siri ambao haukutarajiwa ndio uliokuwa wa hadhi ya juu kati ya Marekani na Korea Kaskazini tangu 2000.
''Tumekuwa na mazungumzo ya moja kwa moja, katika ngazi za juu'', Rais Trump amesema mjini Florida ambapo alikuwa anakutana na waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe.
Rais huyo ameongezea kuwa aliunga mkono mazungumzo kati ya Korea Kusini na Kaskazini kuzungumzia makubaliano ya amani ya kumaliza vita vya Korea vya 1950-1953
Korea Kusini imetoa ishara kwamba itaangazia suluhu rasmi ya kumaliza mgogoro huo. Rais wa Korea Kusini Moon Jae in na Kim wanatarajiwa kukutana mwisho wa mwezi huu Aprili.
Habari kwamba mteule wa rais Donald Trump katika wizara ya masuala ya kigeni alisafiri kueleka Korea Kaskazini kwa mkutano huo na Kim ziliripotiwa mara ya kwanza na gazeti la The Washington Post.
Ni machache yanayojulikana kuhusu mazungumzo hayo mbali na kwamba yalilenga kuwa jukwaa la kuandaa mkutano mwingine wa moja kwa moja kati ya rais Donald Trump na Kim Jong Un.
Kulingaa na gazeti hilo, mkutano huo ulifanyika mara tu baada Pompeo kuteuliwa kuwa waziri wa masuala ya kigeni kulingana na maofisa wawili waliokuwa na habari kuhusu safari hiyo.
Baadaye chombo cha habari cha Reuters kilisema kuwa ripoti hiyo imethibitishwa na maofisa waandamizi. Ikulu ya Whitehouse haijatoa tamko lolote.
Marekani haina uhusiano wa kidiplomasia na Korea Kaskazini lakini wajumbe wa mataifa hayo mawili wametembeleana miaka ya mbeleni na kuna idhaa zinazotumika kuwasiliana na Pyonyang.
Safari ya Pompeo ilikuwa ziara ya ngazi ya juu na kiongozi huyo wa Korea Kaskazini tangu 2000 wakati waziri wa masuala ya kigeni nchini Marekani Madeleine Albright alipokutana na Kim Jong-il, babake kiongozi wa sasa wa Pyonyang.
Mwaka 2014 , kiongozi wa shirika la upepelezi 2014, James Clapper alizuru Korea Kaskazini kisiri ili kujadiliana kuhusu kuachiliwa huru kwa raia wawili wa Marekani .
Clapper hakukutana na kiongozi huyo wa Korea Kaskazini wakati wa ziara hiyo. Rais Trump aliishangaza jamii ya kimataifa kwa kukubali mapendekezo ya Pyonyang ya mazungumzo ya moja kwa moja. Sio kawaida kwa rais wa Marekani kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini.
Amesema mkutano huo utafanyika Julai ama siku chache kabla ya mwezi huo huku maeneo yakiangaziwa na kwamba hakuna hata eneo moja ambalo liko Marekani miongoni mwao.
Wachanganuzi wamedai kwamba eneo la mazungumzo hayo huenda likawa lisilo na majeshi kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini, Beijing, taifa jingine la bara Asia, Ulaya ama hata katika meli iliopo katika maji ya kimataifa.
Korea Kaskazini imetengwa kwa miongo kadhaa kutokana na historia yake ya unyanyasaji wa haki za kibinadamu mbali na utengenezaji wake wa silaha za kinyuklia ikikiuka sheria za kimataifa na vikwazo vya Umoja wa Mataifa.
Imetekeleza majaribio sita ya kinyuklia na ina makombora ambayo yanaweza kufika Marekani.
Lakini maandalizi ya michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi yaliyofanyika Februari nchini Korea Kusini yalitoa dirisha la kidiplomasia na wiki chache baada ya michezo hiyo kumekuwa na ziara kadhaa za Korea Kaskazini kutoka China, Korea Kusini na sasa Marekani.
Rais Trump anakadiria kwamba mkutano huo unaweza kufanyika mwezi Juni ama mapema. Lakini habari za ziara ya Pompeo inatarajiwa kuweka kando uhusiano mzuri kati yake na Japan, ambaye ni mshirika mkuu wa Marekani na jirani wa Korea Kaskazini.
Kumekuwa na hofu mjini Tokyo kwamba  Trump ana mpango wa mazungumzo ya kibiashara ambayo huenda yakaipuuza Japan na Shinzo Abe kwa sasa yuko nchini Marekani kwa mazungumzo na kiongozi huyo wa Marekani.
Uhusiano kati ya wawili hao ulionekana kuwa mzuri kuhusu suala hilo , ikiwa ni mara ya pili kwamba Trump amemkaribisha Abe katika mgahawa wake wa Mar-a-Lago resort.
Trump amesisitiza siku ya Jumanne kwamba mataifa hayo mawili yanashirikiana kuhusu suala la Korea Kaskazini, huku naye Shinzo Abe akimpongeza rais huyo wa Marekani kwa kuliangazia suala la Korea Kaskazini.
Hata hivyo, waangalizi wanasema lengo la Abe ziarani Marekani ni kuishawishi Marekani.
Waziri huyo wa Japan ameonekana kutaka kuonesha uhusiano wa karibu na Rais Trump na alikuwa kiongozi wa kwanza wa kigeni kukutana naye mjini New York baada ya ushindi wake wa uchaguzi wa mwaka 2016.

MKURUGENZI wa Shirika la Upelelezi (CIA), nchini Marekani, Mike Pompeo alisafiri hadi mjini Pyongyang kwa mkutano wa kisiri na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un , kulingana na vyombo vya habari vya Marekani.
Mkutano huo ulioandaliwa kuandaa mkutano mwingine kati ya rais Donald Trump na Kim Jong Un, ulifanyika wikendi ya sikukuu ya Pasaka , kulingana na maofisa ambao hawakutajwa.

No comments:

Post a Comment