Thursday, 5 April 2018

Mkutano wa wawekezaji unaolenga kutia hamasa ya kuanzishwa viwanda vya dawa na vifaa tiba nchini

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akifafanua jambo kwa wadau wa mkutano wa wawekezaji wenye nia ya kuanzisha viwanda vya dawa na vifaa tiba nchini wakati wa mkutano wa wadau hao mapema jana Dar es Salaam.Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akisisitiza jambo kwa wadau wa mkutano wa wawekezaji wenye nia ya kuanzisha viwanda vya dawa na vifaa tiba nchini (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa wadau hao mapema jana Dar es Salaam.Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu akitoa taarifa ya hali ya soko la dawa nchini kwa wadau wa mkutano wa wawekezaji wenye nia ya kuanzisha viwanda vya dawa na vifaa tiba nchini (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa wadau hao uliofanyika jana Dar es Salaam.


Baadhi ya wadau wa mkutano wa wawekezaji wenye nia ya kuanzisha viwanda vya dawa na vifaa tiba nchini wakimsikiliza Mgeni rasmi Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (hayupo pichani) wakati wa mkutano wao mapema jana Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment