Monday, 9 April 2018

Mlonge mti wa maajabu unaotibu maradhi mengi


Mlonge
MLONGE umekuwa ukijulikana kama mti wa miujiza kwa karne nyingi katika baadhi ya nchi za Afrika, Asia na Caribbean. Mti huu umeripotiwa kutibu magonjwa mengi yakiwemo yale sugu.
Tofauti na baadhi ya miti mingine, maajabu ya mlonge yanagawanyika katika makundi matano kwa maana ya majani, maua, magome, mizizi na mbegu.
Majani
Majani ya mlonge yamesheheni virutubisho ambapo vinauwezo wa kuwasaidia wenye matatizo ya kisukari, waathirika wa virusi vya Ukimwi, watu wanaoonekana wazee kabla ya umri wao na kusaidia afya ya damu.
Mlonge ambao pia hujulikana kama mti wa imani tangu enzi za mababu, unaweza kutumia majani machanga kama mboga kila mara au kuyakausha kitaalam kisha kusaga unga wake kijiko kimoja cha chai unaweza kukitumia katika uji mwepesi au maji moto kutwa mara matatu.
Maua
Maua ya mlonge yana nguvu kubwa katika tiba ambapo yanasaidia kinamama wenye tatizo la uzazi kwa kuwa yana uwezo wa kuweka sawa homoni zao na hivyo kupevusha ipasavyo mayai pamoja na kusafisha nyumba ya uzazi.
Chukua kilo moja ya majani hayo yachemshe kisha kunywa glasi moja kutwa mara tatu, au maua makavu yaliyokaushwa kitaalamu saga unga wake utumie kijiko kimoja cha chai katika maji moto au uji mwepesi utathibitisha maajabu yake.
Mbegu 
Mbegu nazo zinafanya kazi ya kutibu maradhi mengi miongoni mwayo ni kuwezesha usanisi wa chakula, wenye maradhi ya kisukari na shinikizo la juu la moyo.
Tumia punje tatu za mlonge kila siku kwa muda wa siku tisa hadi 14 utaona mabadiliko makubwa kiafya.

Magome
Magome ya mlonge yana uwezo mkubwa wa kupandisha CD4 hususan kwa waathirika wa Ukimwi, kwani una kiwango kikubwa cha vitamin A, B1, B3, B6 na B12 wingi huo pia unasaidia kutengeneza afya ya damu.
Pia Mlonge unaweza kuwasaidia wenye matatizo ya vidonda vya ndani, kuulinda mwili na vidonda vya tumbo.
Ili kutumia unapaswa kukausha kitaalamu gome la mlonge kisha saga unga na tumia kijiko kimoja cha chai katika uji mwepesi ua maji moto kutwa mara tatu.

Mizizi
Mizizi ya mti huu wa maajabu inatibu majibu makubwa (tambazi), damu yenye fangasi, inasaidia kuongeza kinga mwilini na hivyo kuboresha afya ya mtumiaji.
Namna ya kuandaa kama ni katika jipu kubwa ponda mizizi kisha iweke katika kitambaa safi funga juu ya uvimbe huku ukihakikisha kuwa dawa hiyo haigusani na ngozi.
Pia unaweza kukausha mizizi kisha unga wake kuutumia katika uji mwepesi au maji moto, unasaidia kutuliza maumivu.
Haya ni miongoni mwa magonjwa machache tu yanayoweza kutibiwa kwa mlonge yapo mengi mengine.
Licha ya maelezo hayo ni vema ukiwa unakabiliwa na tatizo linalohitaji tiba hii njoo makao yetu makuu kupata maelezo ya kina kuhusu mti huu adhimu ambao ni faraji dhidi ya maradhi mengi.
Mchanganuo huu umeletwa kwako na mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho vyetu.

Mbegu za mlonge

No comments:

Post a Comment