Monday, 23 April 2018

Mtopetope unavyoboresha mbegu za uzazi na kuongeza hisia za tendo la ndoaTopetope


DUNIANI kuna aina nyingi za magonjwa miongoni mwayo ni yale yanayoenezwa kwa kufanya ngono.

Magonjwa hayo yamegawanyika katika makundi kulingana na dalili zake ambapo kundi la kwanza ni yale yenye dalili za kutokwa usaha au majimaji sehemu za siri (ukeni au uumeni) kama kisonono, trichomonas na candida.

Kundi jingine ni la magonjwa ya ngono ambayo dalili zake ni kutokwa na vidonda ambayo ni pamoja na kaswende na malengelenge sehemu za siri.

Aidha, kundi la tatu ni la magonjwa yenye dalili za kutokwa uvimbe ambayo ni mitoki na pangusa sehemu za siri (vinyama laini vidogo vinavyoota kwenye ngozi au utando unaozunguka maeneo ya siri.

Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai anasema kujitokeza kwa dalili za ugonjwa wa ngono hutegemeana na aina ya ugonjwa na jinsi kinga ya mwili wa mgonjwa ilivyo.

"Hatari kubwa ya magonjwa haya ni kwa wanawake au watu wa jinsia ya kike, kwani asilimia 60 hadi 70 ya wanawake wenye kisonono hawaoneshi dalili yoyote wakati wanaume ni kati ya asilimia 10 hadi 15," anasema.

Anafafanua kuwa ni muhimu kwa vijana wa kiume akiona dalili za ugonjwa kumweleza mwenzi wake wa kike aliyejamiiana naye ili wote waende kwenye kituo cha huduma za afya kwa uchunguzi na tiba.

"Napenda ieleweke kwamba mtu anaweza kuwa na magonjwa zaidi ya ugonjwa mmoja wa ngono kwa wakati mmoja," anasisitiza.

Anatanabaisha dalili anazoweza kuziona mwanamke iwapo ameambukizwa magonjwa ya ngono ni pamoja na kujisikia maumivu chini ya kitovu au kutokwa na usaha au majimaji yenye harufu mbaya sehemu zake za siri.

Pia anaweza kujisikia kuwashwa sehemu za siri au kutokwa na vidonda na vipele kwenye sehemu hizo, mdomoni au sehemu nyingine za mwili.

"Wakati wa kujamiiana anaweza kusikia maumivu makali au akawa amevimba mitoki, kuota mafundofundo sehemu za siri na kujisaidia haja ndogo mara kwa mara kunakoambana na mwasho au maumivu sehemu hizo," anasema.

Aidha, akibainisha dalili za magonjwa ya ngono kwa wanaume anasema dalili za tatizo hilo kwa wanaume ni kujisikia maumivu makali wakati wa kujisaidia haja ndogo au kutokwa na usaha sehemu ya mbele kwenye uume.

Pia atatokwa na usaha pamoja na kuwa na vidonda sehemu za siri na mdomoni na anaweza kuvimba mitoki na kupata malengelenge sehemu hizo.

Mtaalam Mandai anasema magonjwa hayo huweza kuwapata watu wa rika na jinsia zote huku vijana walio na umri wa kati ya miaka 15 na 49 wapo hatarini zaidi.

Vijana wenye umri wa kati ya miaka 10 hadi 24 wapo katika hatari kubwa zaidi kupata maambukizi ya magonjwa ya ngono kwa kuwa hisia zao za kujamiiana zipo juu zaidi.

Anasema hali hiyo huwapata kwa kuwa homoni au vichocheo vilivyomo mwilini mwao husababisha hisia za kufanya ngono.

Mandai ana utaja mti wa mtopetope ambao unapatikana katika mikoa mingi hapa nchini kuwa unasaidia kupambana na maradhi hayo.

Anasema mti huo wa asili unaostawi sehemu zenye maji na kame, umeonesha uwezo mkubwa wa kupambana na maradhi mengi na unasifika kwa kuwa kikubwa kikubwa cha madini ya calsium.

Anafafanua kuwa ganda la mtopetope likipondwa na kubandikwa kwenye uvimbe au kama ndani ya utumbo kuna uvimbe mgonjwa akanywa majani yake yaliyochemshwa unatoweka kabisa.

Pia anasema mti wa mtopetope una kinga nyingi kutokana na kuwa na kiasi kikubwa cha protini. Mandai anatanabaisha kuwa mtopetope pia unaboresha mbegu za uzazi na hivyo kuongeza hisia za tendo la ndoa.

"Kijiko kimoja cha unga wa majani ya mti huu, unaweza kuchanganya na maji ya moto unakunywa asubuhi, mchana na jioni ni kinga moja nzuri sana ya magonjwa mbalimbali, asubuhi ni vema ukanywa kabla ya kula,” anasema.

Mtaalam huyo ambaye amepata uzoefu wa masuala ya tiba kwa kutumia mimea kutoka katika mataifa kadhaa ya Afrika, amesaidia wengi wanaokabiliwa na matatizo mbalimbali ya kiafya.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho tiba vyetu.

No comments:

Post a Comment