Saturday, 28 April 2018

Musiba hakufukuzwa bungeni


Cyprian Musiba

Mary Meshack, Dodoma

BUNGE limekanusha taarifa zilizodai kuwa Mkurugenzi wa CZI,  Cyprian Musiba amefukuzwa bungeni.

Taarifa hizo ziliibuka mara baada ya kuwepo picha mtandaoni ikimuonesha Musiba 'akizozana' na baadhi ya watumishi wa Bunge. Kupitia ukurasa wa Twitter wa Bunge wamefafanua kuhusiana na hilo;

Picha zinazosambaa kwenye mitandao zikidai kuwa Mkurugenzi wa CZI  Cyprian Musiba amefukuzwa Bungeni si  kweli.  Musiba  amekidhi vigezo vya kusajiliwa kuripoti habari za Bunge na kwamba alikuwa akihamishwa kwenda katika jukwaa mahsusi ambalo wanahabari hukaa wawapo bungeni.

Musiba ni mhariri wa Gazeti la Tanzanite na mwanasheria, hivi karibuni alifunguliwa kesi na Mjasiriamali/Mwanahabari na Mkurugenzi wa Compass Communications, Maria Sarungi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa madai ya kumkashifu na kuchafua jina lake kupitia mkutano wake na wanahabari uliyofanyika February 25, mwaka huu (2018).

No comments:

Post a Comment