Tuesday, 10 April 2018

Musukumu azidi kuishauri serikali kuendelea kuwapa ajira wasio na cheti ya ufaulu kidato cha nneJoseph Kasheku (Musukuma)


MBUNGE wa Geita vijijini, Joseph Kasheku (Musukuma) amesema serikali iendelee kuwatambua watu wenye elimu ya darasa la saba ikiwa ni pamoja na kuwapatia ajira ambazo wanazimudu.

Kauli ya Musuku inakuja mara baada ya serikali kuamuru kurudishwa kazini kwa Watumishi wote ambao walikuwa na ajira za kudumu au ajira za mikataba (kwa watendaji wa vijiji na mitaa) au ajira za muda ambao walikuwa kazini kabla ya Mei 20, 2004 ulipoanza kutumika waraka wa Utumishi Na. 1 wa mwaka 2004 ambao umetaja kuwa cheti cha ufaulu wa mtihanai wa kidato cha nne kama sifa ya msingi kwa mtumishi wa umma. 

Akizungumza leo mjini Dodoma na kituo cha runinga cha Azam, Musukuma ametolea mfano madereva wenye elimu ya darasa la saba kwa kueleza hakuna sababu ya serikali kuwatenga katika ajira ikiwa chuo cha NIT kinawapokea.  

"Tunachoshauri serikali iendelee kuwatambua watu wa darasa la saba, kwenye kazi ambazo wanastahili kufanya. Napenda kutoa mfano kwenye tasnia ya udereva, chuo cha NIT kinachukua wa darasa la saba na graduate," amesema.

"Inakuwaje NIT inachukua kodi ya watu darasa la saba halafu kwenye ajira serikali inawatoa. Watu wa darasa la saba hawakuwa na makosa kuishia hapo na wao ni mipango yao pamoja na kwamba fursa ya kusoma ilikuwepo lakini Chuo Kikuu hakiwezi kuchukua watu wote," amesisitiza.

Jana April 09, 2018 bungeni Mjini Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni Mstaafu George Mkuchika amesema watumishi wa Umma 1,370 waliolegezewa masharti ya sifa za muundo kupitia barua ya Katibu Mkuu Utumishi yenye Kumb. Na. CCB.271/431/01/p/13 ya Juni 30 , 2011 warejeshwe kazini mara moja, walipwe mishahara yao kwa kipindi chote ambacho walikuwa wameondolewa kazini na waendelee na ajira zao hadi watakapostaafu kwa mujibu wa Sheria.

No comments:

Post a Comment