Tuesday, 17 April 2018

Mwanaume aliyemtupa mwanawe kutoka paa la nyumba ashtakiwaRAIA wa Afrika Kusini ameshtakiwa mahakamani kwa unyanyasaji wa mtoto baada ya kumtupa binti yake wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja kutoka juu ya paa la nyumba yake wiki iliopita.

Mashtaka yake yalipunguzwa kutoka jaribio la kutaka kuua, kulingana na mwandishi mmoja wa shirika la habari la eNCA aliyetuma ujumbe wa Twitter.

Mtu huyo mwenye umri wa miaka 38 alichukuliwa katika kanda ya video akimrusha mtoto huyo wakati wa maandamano dhidi ya uvunjaji wa mitaa ya mabanda katika mji wa pwani wa Port Elizabeth.

Gazeti moja la eneo hilo lilituma ujumbe wa Twitter wa picha ya ofisa wa polisi akimkamata.
Polisi walikuwa wakivunja vibanda 150 katika makazi ya Joe Slovo ambayo wanasema yalijengwa katika ardhi iliyokaliwa kinyume na sheria.

Mtu huyo ambaye nyumba yake ndio iliokuwa haijavunjwa , alisaidiwa kupanda juu ya paa na mwanamke aliyeripotiwa kuwa mama wa mtoto huyo.

Alikuwa juu ya paa hilo kwa takriban dakika tano kabla ya kumtupa huku wakazi wengine wakipiga kelele ''mtupe, mtupe, mtupe'' kulingana na jarida la Herald. Mtu huyo ambaye bado hajaulizwa kujitetea amewekwa kizuizini.

No comments:

Post a Comment