Tuesday, 3 April 2018

Naibu Spika aapisha wabunge wapya


Maulid Mtulia akiapa mbele ya Naibu Spika Tulia Ackson (hayupo pichani),  bungeni leo mjini Dodoma.

NAIBU Spika, Tulia Ackson, leo (Aprili 3, 2018) amewaapisha wabunge wawili, Dk. Godwin Mollel wa Siha na Maulid Mtulia wa Kinondoni.

Wabunge hao wameapishwa baada ya kufanyika kwa uchaguzi mdogo katika majimbo ya Siha na Kinondoni,  baada ya wabunge wa maeneo hayo kuhamia CCM.

Mtulia, alikuwa mbunge wa Kinondoni (CUF), kabla ya kuhamia CCM na kugombea tena jimbo hilo kwa kupitia CCM.

Kadhalika Mollel, alikuwa mbunge wa Siha, (Chadema) kabla ya kuhamia CCM na kugombea tena jimbo hilo kwa tiketi ya CCM.

Hata hivyo kiapo hicho hakikushuhudiwa na idadi kubwa ya wabunge wa upinzani ambao hawakuwepo katika kikao cha leo. Hili ni bunge la 11 na mkutano 11.

No comments:

Post a Comment