Saturday, 28 April 2018

Ndizi zinavyosaidia kuamsha uwezo wa uelewa kwa mwanafunzi


Ndizi mbivu

NDIZI ni miongoni mwa matunda maarufu sana hapa nchini yanayopendwa na wengi kutokana na radha yake tamu.

Ni tunda maarufu kwa sababu linastawi katika maeneo mengi nchini licha ya kuwa ipo mikoa kama Mbeya, Kagera na Kilimanjaro ambayo inastawisha kwa wingi zaidi zao hilo.

Katika baadhi ya maeneo huzitumia ndizi hususan mbichi kama chakula huku wengine wakizitumia mbivu kama tunda.

Kwenye mikoa ambayo zao hilo linastawishwa kwa wingi limekuwa likitumiwa kama chakula kikuu kwa familia na jamii nzima.

Hata hivyo, wakati baadhi wakitumia ndizi kama chakula au tunda bila kujua faida zake katika mwili wa binadamu, Mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai anasema ndizi ina maajabu makubwa katika tiba.

"Ndizi ina aina tatu za kipekee za sukari zinazojulikana kitaalamu kama sucrose, fructose na glucose na vilevile ina kiasi kingi cha ufumwele (fible) ambacho husaidia katika usagaji wa chakula tumboni.

"Ndizi ina uwezo mkubwa wa kuongeza na kuimarisha nishati ya mwili. Unaweza kupata nishati ya kufanyakazi kwa muda wa dakika 90 kwa kula ndizi mbili tu. Bila shaka ndizi ni tunda muhimu kwa wanamichezo.

"Hata hivyo, nishati siyo faida pekee unayoweza kuipata katika ndizi, ni tunda lenye uwezo pia wa kuponya na kuzuia matatizo mengi ya kiafya," anasema.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Chama cha Afya ya Akili cha Taifa (Mindi) cha Uingereza kwa watu wanaosumbuliwa na tatizo la mfadhaiko wa akili, watu wengi waliondokana na tatizo na kujisikia vizuri baada ya kula ndizi mbivu.

Hali hiyo inatokana na ukweli kwamba ndizi ina kirutubisho kinachojulikana kama tryptopham ambacho ni aina fulani ya protini inayotumika mwilini humfanya mtu kuwa mtulivu na mwenye furaha.

Manda anasema wanawake wanaokabiliwa na changamoto mbalimbali wakati wa hedhi wanashauriwa kula ndizi mbivu wanaweza kuondokana na matatizo hayo ya kiafya.

"Vitamini B6 iliyomo kwenye ndizi, hurekebisha kiwango cha sukari ambacho huweza kuathiri hali ya mtu," anatanabaisha.

Anasema kwa mwenye changamoto ya upungufu wa damu ndizi ni chanzo kizuri cha madini aina ya chuma (iron), hivyo kwa mwenye tatizo hilo ale tunda hilo kwa kuwa ni dawa ya kuzuia na kuponya upungufu wa damu kwa sababu ya madini ya chuma ambayo yanaamsha uzalishaji wa chembechembe za damu mwilini.

Kwa mwenye shinikizo la damu anasema tunda hilo ni la kipekee ambalo lina kiwango kikubwa cha madini ya potassium na wakati huo huo lina kiasi kidogo sana cha chumvi hivyo kulifanya kuwa tunda bora katika kupambana na tatizo la kupanda na kushuka kwa shinikizo la damu.

Anasema kiwango kidogo cha chumvi kilicho katika ndizi kinalifanya tunda hilo kuwa bora katika kupambana na tatizo la kupanda na kushuka kwa shinikizo la damu.

Ukweli huo umeifanya Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini Marekani iwaruhusu wazalishaji na wauzaji wakubwa wa ndizi nchini humo, kutangaza rasmi uwezo wa ndizi katika kupambana na hatari ya shinikizo la damu na kupatwa na kiharusi kwa binadamu.

Hivi karibuni kulikuwa na taarifa kuwa wanafunzi 200 kwenye Shule ya Tickenham nchini Uingereza, walifaulu vizuri mitihani yao baada ya kula ndizi mbivu baada ya mlo wa asubuhi, muda wa mapumumziko na wa chakula cha mchana. Ndizo ziliwaongezea uwezo wa kufaulu.

"Utafiti unaonesha kuwa wingi wa potassium katika ndizi una uwezo wa kumsaidia mwanafunzi kuamsha uwezo wa kumfanya awe na uelewa mkubwa katika masomo yake," anasema Mtaalam Mandai.

Akizungumzia kuhusu uchovu wa mwili anasema moja ya dawa za haraka ambazo zinasaidia kuondoa hali hiyo ya uchovu unaotokana na ulevi wa jana ni kunywa 'milkshake' iliyotengenezwa kwa ndizi na kutiwa asali.

"Ndizi hutuliza tumbo, ikisaidiwa na asali, hurejesha kiwango cha sukari kilichopungua kwenye damu wakati maziwa hutuliza na kurejesha maji kwenye mfumo wake," anatanabaisha mtaalamu huyo.

Anasema ndizi husaidia katika matatizo mengine mengi ya kutuliza mishipa ya fahamu, kuondoa wasiwasi, kutuliza vidonda vya tumbo asidi tumboni, kushusha joto mwilini na kurekebisha mapigo ya moyo.

"Hivyo, ndizi ni tiba ya magonjwa mengi na ni bora ukilinganisha na tufaa (aplle), ndizi ina protini mara nne zaidi, wanga mara mbili zaidi, vitamini A na chuma mara tano na madini mengine mara mbili zaidi ya tufaa," anafafanua.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho vinavyozalishwa na kampuni yetu.

No comments:

Post a Comment