Sunday, 8 April 2018

Nyumba za Polisi zimenipa mke - Rais Magufuli


RAIS Dk. John Maguli amesema Jeshi la Polisi ndilo lilimpa mke aliye naye sasa, Mama Janeth Magufuli baada ya baba yake kuwa askari polisi hadi mauti yalipomfika.


Rais ameyasema hayo jana Jumamosi, Aprili 7, 2018 baada ya kuzindua kituo cha polisi cha Kidiplomasia na Utalii  eneo la Naura jijini Arusha na baadaye nyumba 31 za polisi zilizojengwa kwa ushirikiano wa serikali na wafanyabiashara baada ya zilizokuwepo kuungua moto Septemba mwaka jana.

“Nyumba za polisi nazifahamu vizuri sana, ndiyo zilizonipa mke, huyu mke wangu baba yake alikuwa polisi, na mpaka amekufa wala hakuwa na cheo, alikuwa ‘staff sergeant’, kwa hiyo maisha ya polisi ninayafahamu na yamenitunzia mke.

“Ningekuwa nazindua nyumba kama hizi huko Moshi, angenionesha nyumba waliyoishi lakini za Oyster Bay alizoishi alishanionesha na za Ukonga na za sehemu nyingine. Kwa hiyo maisha ya polisi ninayafahamu, Hivyo, polisi mna msemaji mwingine ambaye ni mke wangu ukiachilia mbali Waziri wa Mambo ya Ndani (Mwigulu) na IGP Sirro,” amesema Rais Magufuli.

No comments:

Post a Comment