Saturday, 7 April 2018

Papai tunda tamu linalosaidia matatizo mengi kiafya


Papai lililowiva

PAPAI ni tunda lenye ladha tamu inayovutia wengi kulila. Asili ya papai ni Amerika Kusini na Kati. Mpapai (mti wa papai), una shina lenye urefu wa mita 5 hadi 10. Tunda hili lina vitamini A, B, C, D na E.

Kula mbegu za papai mkono mmoja usiojaa sana utaua vidudu wote tumboni. Tunda binti la papai baada ya kuondoa ganda, pika nyama yake nyeupe na ule kila siku asubuhi na jioni kwa muda wa wiki moja (siku saba), linasaidia sana kwa wanaosumbuliwa na homa ya manjano.

Majani ya mpapai yanasaidia kwa mtu aliyekula sumu katika chakula au tumbo lililochafuka au mtu aliyekula chakula kibaya. Twanga majani kiasi cha kujaza mkono mmoja, weka katika maji na unywe. Utatapika au utapona baada ya matumizi hayo.

Papai pia linasaidia kwa mtu mwenye shida ya usanisi wa chakula tumboni kutofanyika kwa ufasaha, tatizo la kisukari na asthma, kifua kikuu, maziwa yanayotoka bila mpangilio ambapo jani la papai husaidia tatizo hilo, matatizo ya kiungulia, kutofunga choo na kikohozi cha mapafu.

Pia papai linasaidia afya nzuri linapotumiwa kila siku, linasaidia tatizo la njia ya choo kubwa kwa ndani, maganda yake yanasaidia kwa mwenye tatizo la kuungua moto, vipele na saratani ya ngozi.

Hata hivyo, iwapo utakumbwa na moja ya matatizo tajwa ni vema ukatembelea makao yetu makuu kupata maelezo ya kina ya namna ya kutumia papai kutatua tatizo lako kiafya.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment