Tuesday, 3 April 2018

Penda kula ndizi ni kinga ya magonjwa


Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai akizungumzia umuhimu wa kula matunda zikiwemo ndizi kwa kuwa yanafaida nyingi katika miili ya binadamu.

ASILI ya migomba (ndizi) ni maeneo ya Kusini mwa Asia, hapo awali inaonesha ilikuwa huko Papua New Guinea. Leo ndizi hustawishwa kwenye zaidi ya nchi 107 duniani.

Ndizi zina vitamin A, B, C, E na G, ndani yake kuna madini ya potassium, calcium, sodium, magnesium, silicon, phosphorous, sulphuur na chlorine.

Ndizi mbivu mara nyingi zinatumika kama matunda, wakati zile mbichi zinatumika kama chakula huku katika baadhi ya maeneo katika nchi za Afrika Mashariki yakitumia kama chakula kikuu.

Zina faida nyingi katika mwili wa binadamu ikiwemo kupigana na magonjwa ambayo huja kwa kukusanyika maji mwilini au yanayofanana na hayo.

Tunda hilo pia humsaidia mtu mwenye tatizo la maumivu ya tumbo au mwili mzima, watoto pia inawasaidia sana. Zinatuliza na kuponya maradhi mengi ya tumbo.

Ndizi pia zinasaidia kupambana na maradhi ya TB hususan unapokula kwa uaminifu. Pia huponya magonjwa ya kuvimba mwili, matatizo ya utumbo mwembamba, matatizo ya neva na maumivu ya kifua.

Pia tunda hili huweza kusaidia kupunguza unene, iwapo utaacha kutumia chakula kingine ila ndizi pekee, au unaweza kutumia kila baada ya mlo katika milo mitatu unayokula kwa siku.

Ndizi pia zinasaidia kusafisha damu hasa ile inayochafuliwa na asidi au mlo usio na mpangilio.

Hata hivyo, ni vema ndizi zisitumiwe kwa wingi zaidi kwa wakati mmoja licha ya kuwa ni rahisi kuyeyushwa mwilini.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho vyetu.

No comments:

Post a Comment