Thursday, 26 April 2018

Penda kutumia zabibu zinalinda afya ya mfumo wa damu


Mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai akizungumzia umuhimu wa jamii kujenga utaratibu wa kutumia zabibu kwa kuwa zina faida nyingi katika mwili wa binadamu.


MZABIBU (mti wa zabibu) unaotoa matunda yanayojulikana kama zabibu si maarufu sana hapa nchini kwa sababu hustawishwa katika mikoa michache. 

Zabibu zinatumika kutengenezea vyakula na vinywaji mbalimbali ukiwemo mvinyo ambao ni kinywaji maarufu duniani.

Tunda hilo ambalo huliwa kama lenye kama yalivyo matunda mengine, mara nyingi linakuwa katika kichana chenye zabibu 6 hadi 300. Watafiti wa zao hilo wanasema tunda hilo lilianza kustawishwa nchini Uturuki, hapa nchini linastawishwa kwa wingi mkoani Dodoma.

Matunda yana rangi nyekundu iliyowiva, nyeusi, bluu ya kukoza, njano, kijani na pinki. Hapa nchini yanapatikana kwa wingi yale yenye rangi ya bluu iliyokoza.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo Duniani (FAO), linasema asilimia 71 ya zabibu yote duniani hutumika kutengenezea mvinyo na asilimia 27 huliwa kama matunda ya kawaida, huku asilimia 2 ikikaushwa.

Mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai anasema zabibu husaidia kuupa mwili nguvu na kuimarisha afya ya mishipa ya damu hususan ile inayosambaza damu kwenye nyama ya moyo.

Anasema zabibu pia husaidia damu kuwa nyepesi na kuzuia isigande ndani ya mishipa yake, hivyo kutokana na sababu hiyo hupunguza hatari ya kukubwa na kiharusi.

Anafafanua kuwa zabibu inasaidia kuzuia na kutibu tatizo la upungufu wa damu na kwa wale wanaotumia mara kwa mara tunda hilo huwasaidia kuepukana na ugonjwa wa bawasili.

Mtaalamu huyo anasema matunda hayo husaidia katika tiba na kinga ya magonjwa ya ini kutokana na uwezo wake wa kuliongezea ini uwezo wa kuondoa sumu mwilini na kuzalisha nyongo kwa wingi.

Mandai anaongeza faida nyingine ya zabibu ni kuimarisha afya ya figo na kuifanya kuwa na uwezo zaidi wa kuondoa sumu katika damu.

"Faida nyingine ya zabibu inasaidia kupunguza uchovu wa mwili na kutibu maumivu yasiyokuwa na sababu za moja kwa moja kutokana na tunda hilo kuwa na sukari yake ya asili.

Sanjari na hayo, mtaalam huyo anasema juisi ya zabibu (divai) husaidia tumbo na utumbo kufanya kazi vizuri na kuzuia ukavu wa haja kubwa.

Anataja faida nyingine ya divai ni kwamba ina uwezo mkubwa wa kuimarisha afya ya mishipa ya damu katika mfumo wa kumeng'enya, kusaga na kusharabu chakula na viini lishe.

Divai pia husaidia bakteria rafiki kwa binadamu wanaoishi ndani ya tumbo kukua vizuri na kusababisha umeng’enyaji wa chakula ndani ya tumbo kuwa rahisi.

Mandai anasema katika zabibu kuna madini ambayo huifanya divai kuwa dawa nzuri inayopunguza maumivu ya tumbo yanayotokana na kujiminya kwa misuli ya kuta za matumbo.

Mtaalam huyo anasisitiza matumizi ya zazibu japo punje zisizopungua tano kwa siku ili kulinda afya ya mfumo wa damu na nyama ya moyo.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho vinavyozalishwa na kampuni yetu.

No comments:

Post a Comment