Wednesday, 25 April 2018

Polisi Arusha yawatia mbaroni washukiwa wa kuhamasisha maandamano


Kamishna msaidizi mwandamizi, Yusuph Ilembo 

Mwandishi Wetu, Arusha

JESHI la Polisi mkoani Arusha linawashikilia watu saba wakishukiwa  kuhamasisha maandamano yanayodaiwa kufanyika Aprili 26, mwaka huu.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha , Kamishna msaidizi mwandamizi, Yusuph Ilembo amesema washukiwa hao wamekuwa wakihamashisha maandamano kupitia mitandao ya kijamii ikiwapo Telegram na WhatsApp.

Amesema watu watatu kati ya hao saba ni wanafunzi wa vyuo vikuu na walitiwa nguvuni na jeshi hilo mara baada ya kufanya upelelezi wa kiitelejensia na kubaini ushawishi waliokuwa wanaufanya kupitia mitandao hiyo.

"Nasisitiza hakuna maandamno Aprili 26, atakayeandamana atavuna alichopanda kwa kuwa serikali haijaribiwi," amesisitiza Ilembo.

No comments:

Post a Comment