Thursday, 19 April 2018

Polisi Mbeya yawatia nguvuni washukiwa wa wizi wa vyombo vya muziki kanisaniMwandishi Wetu, Mbeya


JESHI la Polisi mkoani Mbeya limewatia nguvuni watu watatu kwa tuhuma za wizi wa vyombo vya muziki na viti makanisani mkoani humo.

Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi hilo mkoani hapa limewataja, watu hao kuwa ni William Sanke (23) mkazi wa Isanga, Eliudi Mwansule (28) mkazi wa Mwakibete Viwandani na Noa Molela (26) mkazi wa Kwa Mama John.

Walitiwa nguvuni baada ya misako iliyofanyika katika maeneo mbalimbali ambayo imefanikisha kupatikana mali mbalimbali za wizi ambazo ni spika kubwa 15 za aina mbalimbali, mixer nane, amplifier moja, viti vya plastic 108 vya rangi mbalimbali.

Baada ya kukamatwa na kuhojiwa, watuhumiwa walikiri kuhusika katika matukio ya kuvunja na kuiba makanisani nyakati mbalimbali na mara baada ya kuiba mali hizo huwapelekea wauzaji ambao pia wamekamatwa.

Watuhumiwa wote wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

No comments:

Post a Comment