Wednesday, 25 April 2018

Polisi wazua taharuki mji wa Moshi


Mwandishi Wetu, Moshi


JANA April 24, 2018 saa za asubuhi, Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro limefanya mazoezi kwa vitendo katika baadhi ya maeno ya mji wa Moshi kitu kilichozua taharuki kwa wakazi wa maeneo hayo.

Taarifa kutoka Moshi zinasema shughuli katika mji huo leo zimesimama kwa muda kutokana na mazoezi hayo ambapo polisi walikuwa na silaha za moto.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Hamis Issah amesema zoezi hilo ni la kawaida kwa askari Polisi na kwamba wamekuwa wakipata mafunzo ya nadharia kwa muda mrefu sasa wameamua kuyafanya kwa vitendo.

No comments:

Post a Comment