Tuesday, 24 April 2018

Professor Jay ahoji uhalali wa CCM kumiliki viwanja vikubwa vya michezo


Joseph Haule ‘Professor Jay’ 

Mary Meshack, Dodoma

MBUNGE wa Mikumi, Joseph Haule ‘Professor Jay’ (Chadema) amehoji sababu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kuendelea kumiliki viwanja vikubwa vya michezo wakati kuna uhaba wa viwanja hivyo kwa wanamichezo.

Akiuliza swali Bungeni jana April 23, 2018 amesema tatizo la wanamichezo wa Tanzania ni viwanja kukosa ubora na anafikiri sh. trilioni 1. 5 (zinazodaiwa kupotea) zingeweza kupunguza changamoto hiyo.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amesema sera ya michezo ya mwaka 1995 inahamasisha wadau, vyama, taasisi kumiliki viwanja vya michezo.

“Kwa hiyo viwanja vyote vinamilikiwa kwa uhalali, ni haki yao na hakuna kiwanja hata kimoja kimeporwa na Chama cha Mapinduzi,” amesema Shonza.

Utakumbuka April 20, 2018 wakati Rais Magufuli akiwaapisha majaji Ikulu Dar es Salaam alisema katika ripoti aliyopokea kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad haikuwa na upotevu wa sh. trilioni 1.5 kama inavyodaiwa.

No comments:

Post a Comment