Friday, 13 April 2018

RC Makonda afanya mazungumzo na balozi wa Ufaransa nchini

RC Paul Makonda (kushoto), wakipeana mikono na balozi, Federic Clavier ofisini kwake leo Dar es Salaam. 

Peter Simon

MKUU wa mkoa (RC), wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekutana na balozi wa Ufaransa nchini na kujadili kuhusu kongamano la uchumi litakalofanyika Jumatatu ijayo, Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Makonda amemshukuru balozi huyo na kueleza kuwa wamekuwa marafiki wazuri na Serikali ya Tanzania.


Aidha, kuuhusu kongamano hilo Makonda amesema siku ya Jumatatu kampuni 30 kutoka Ufaransa zitawasili nchini na kufanya mkutano wenye lengo la kulifanya jiji la Dar es Salaam kuwa kama majiji mengine duniani katika masuala ya maji, afya, usafiri na teknolojia.


Ameeleza kuwa kampuni hizo zitaangalia fursa na vipaumbele vya serikali watakavyovitumia katika kuleta maendeleo na ametoa rai kwa wafanyabiashara wa jiji la Dar es Salaam kuja katika ofisi zake kujifunza na kuunganishwa na wafanyabiashara hao kutoka Ufaransa ili waweze kujifunza na kujenga urafiki katika masoko ya bidhaa zao.


Naye Balozi wa Ufaransa nchini, Federic Clavier amefurahia na kumshukuru mkuu ya mkoa Dar es Salaam na kueleza kuwa Dar es Salaam ni mji unaoendelea kukua kiuchumi sanjari na dhamira ya Rais dk. John Magufuli ya kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.


Amesema mkutano huo utakuwa na faida baina ya nchi hizo mbili hasa katika kubadilishana teknolojia katika sekta mbalimbali hasa kwa kuangalia afya, maji pamoja na miundombinu na amehaidi matokeo mazuri yenye faida kwa nchi hizo.


Kuhusu zoezi la kusaidia watoto waliotelekezwa, Makonda amewashukuru wanahabari kwa kuwa sehemu ya wapatanishi wa familia hizo aidha amewataka wananchi kuja kupata huduma katika viwanja vya ofisi yake na sio katika simu na mitandao na ameeleza kuwa hadi sasa familia 178 wameelewana na kukubaliana kupeana fedha za matunzo na zaidi ya watu 1498 wameshapatiwa huduma na siku ya Jumatatu wataitwa baba wa familia hizo licha ya baadhi yao kuanza kuripoti na ameeleza kuwa walio 

No comments:

Post a Comment