Friday, 13 April 2018

Serikali itaendelea kumwenzi Sokoine - Waziri Mkuu Majaliwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na mjane (mke mkubwa) wa marehemu Edward Sokoine Bibi Napono Sokoine, mara baada ya kuwasili nyumbani kwao kushiriki ibada ya kumbukumbu ya miaka 34 ya kifo chake iliyofanyika jana Alhamisi  Aprili 12, 2018. Kulia ni mke mdogo wa marehemu Bibi  Nekiteto Sokoine.


Mjane mkubwa wa hayati Edward Sokoine, Bibi Napono Sokoine, akimvisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mgolole wa Kimasai ikiwa ni ishara ya kumkaribisha nyumbani kwao, kijiji cha Engwiki, kata ya Monduli Juu, wilayani Monduli, mkoani Arusha jana Alhamisi Aprili 12, 2018.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha maombolezo ya hayati Edward  Sokoine kabla ya kuanza ibada ya kumbukumbu ya miaka 34 ya kifo chake iliyofanyika Alhamisi,  Aprili 12, 2018.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwaongoza viongozi wa mkoa wa Arusha na wa Serikali kuimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza ibada ya kumbukumbu ya miaka 34 ya kifo cha hayati Edward Sokoine iliyofanyika jana Alhamisi Aprili 12, 2018.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwasalimia wanafamilia baada ya kutoa salaam zake kwa wananchi waliohudhuria ibada ya kumbukumbu ya miaka 34 ya kifo chake iliyofanyika jana Alhamisi Aprili 12, 2018.

No comments:

Post a Comment