Wednesday, 11 April 2018

Serikali: Tunachukua hatua tunapobaini tangazo lina athari kwa jamii


Juliana Shonza. 

SERIKALI imesema zipo hatua mbalimbali zinazochukuliwa inapobainika kampuni au taasisi imechapisha au kutoa tangazo lenye athari kwa jamii hususan watoto.

Hatua mojawapo ambazo zitachukiwa na serikali ni pamoja na kutoa onyo, kufungiwa kutoa huduma kwa kipindi kitakachotajwa au kufungiwa kutojihusisha kabisa na utangazaji.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amesema hayo jana bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Mororogo Kusini, Prosper Joseph Mbena.

Mbena aliyehoji kwamba  baadhi ya matangazo hayo huwakera na kuleta hisia tofauti kwa baadhi ya watu hasa watoto kutokana na maudhui mabaya.

“Serikali tayari ina vyombo vya kusimamia maudhui ya vyombo vya habari nchini yakiwepo maudhui katika matangazo vyombo hivyo ni mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA)ambayo iliundwa na Kamati ya Maudhui ya kifungu namba 26, Kamati hii inayosimamia maudhui na matangazo ya Kielekronic yaani redioni na televisheni pamoja na mitandao ya kijamii.

“Chombo cha pili ni bodi ya Filamu Tanzania ambayo inasimamia maudhui katika picha jengezi zinazooneshwa katika jumba la sinema, hadharani vilevile katika michezo ya kuigiza 

" Idara ya Habari Maelezo ni chombo cha tatu ambacho kimewekwa chini ya kifungu cha sheria namba nne cha sheria ya habari namba 12 ya mwaka 2016 kinachosimamia maudhui katika machapisho mbalimbali yakiwemo magazeti, majarida pamoja na vipeperushi.

“Zipo hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali inapobainika bila kutia shaka kuwa kampuni au taasisi imechapisha au kutoa tangazo lenye athari kwa jamii

"Serikali inaendelea kuhimiza jamii nzima kuzingatia sheria na taratibu zilizopo katika kusambaza habari mbalimbali kwa jamii,” amesema.

No comments:

Post a Comment