Friday, 13 April 2018

Serikali ya Poland yafungua rasmi ubalozi wake nchini


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk. Augustine Mahiga na Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland, Jacek Czaputowicz wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Ofisi za Ubalozi wa Poland hapa nchini. 

Ufunguzi wa ofisi za ubalozi huo zilizopo Masaki, Dar es Salaam ulifanyika Aprili 12, 2018. Ili kuimarisha na kukuza ushirikiano kati ya Tanzania na Poland, nchi hiyo ilifungua tena ubalozi wake hapa nchini mwaka 2017 baada ya kuufunga mwaka 2008 na kabla ya uzinduzi wa ofisi hizo hapo nchi hiyo ilikuwa inawakilishwa kutokea Nairobi, Kenya. 


Waziri Mahiga akimpongeza Waziri Czaputowicz kwa uamuzi wa nchi hiyo kufungua ofisi za ubalozi wake hapa nchini. 


Waziri Mahiga na mwenzake Czaputowicz wakizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa ufunguzi wa ofisi za Ubalozi wa Poland nchini.


Mkutano kati ya Waziri Mahiga na Czaputowicza na waandishi wa habari ukiendelea.

No comments:

Post a Comment