Sunday, 8 April 2018

Serikali yapata mkopo wa sh. bilioni 34 kutoka mfuko wa maendeleo ya kiuchumi wa Kuwait

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango (Sera), Dk. Khatibu Kazungu (kushoto) na kiongozi wa ujumbe wa wataalamu na mshauri wa masuala ya kilimo wa mfuko wa maendeleo ya kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), Dk. Abdulrida Bahman, wakibadilishana rasimu ya mkataba wa mkopo wa dola milioni 15.3 za Marekani, kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma.


Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango (kulia), akiagana na kiongozi wa ujumbe wa wataalamu na mshauri wa masuala ya kilimo wa mfuko wa maendeleo ya kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), Dk. Abdulrida Bahman, baada ya tukio la kusainiwa rasimu ya mkataba wa mkopo wa dola milioni 15.3 za Marekani, kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji katika bonde la Luiche, mkoani Kigoma, tukio lililofanyika mjini Dodoma wiki hii.
Ujumbe wa wataalamu kutoka mfuko wa maendeleo ya kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), ukiongozwa na  Dk. Abdulrida Bahman (wa tano kutoka kulia), na ujumbe kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango (wa nne kutoka kulia), wakiwa katika picha ya pamoja nje ya Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Mjini Dodoma, baada ya tukio la kusainiwa rasimu ya mkataba wa mkopo wa dola milioni 15.3 za Marekani, kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji katika bonde la Luiche, mkoani Kigoma.


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango (Sera), Dk. Khatibu Kazungu (kulia) akisaini rasimu ya mkataba wa mkopo wa dola milioni 15.3 za Marekani kutoka mfuko wa maendeleo ya kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji katika bonde la Luiche, mkoani Kigoma.


Ujumbe wa wataalamu kutoka mfuko wa maendeleo ya kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), ukiongozwa na  Dk. Abdulrida Bahman (kushoto), wakisikiliza maelezo kutoka kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango (hayupo pichani), kabla ya tukio la kusainiwa rasimu ya mkataba wa mkopo wa dola milioni 15.3 za Marekani, kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji katika bonde la Luiche, mkoani Kigoma.


Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango (kulia), akiongoza mazungumzo kabla ya tukio la kusainiwa rasimu ya mkataba wa mkopo wa dola milioni 15.3 za Marekani, sawa na zaidi ya sh. bilioni 34 kutoka mfuko wa maendeleo ya kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji katika bonde la Luiche, mkoani Kigoma.


Kiongozi wa ujumbe wa wataalamu na mshauri wa masuala ya kilimo wa mfuko wa maendeleo ya kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), Dk. Abdulrida Bahman, akitia saini rasimu ya mkataba wa mkopo wa dola milioni 15.3 za Marekani, kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma.Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango (kulia), akiagana na mmoja wa wajumbe kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), Dk. Abdulrida Bahman, baada ya kusainiwa rasimu ya mkataba wa mkopo wa dola milioni 15.3 za Marekani, sawa na zaidi ya sh. bilioni 34.4, kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma, tukio hilo limefanyika mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment