Friday, 6 April 2018

Sikufahamu kuhusu malipo kwa Stormy Daniels - Trump


Rais wa Marekani, Donald Trump
RAIS wa Marekani, Donald Trump amesema hakufahamu kuhusu malipo ya fedha za Kimarekani 130,000 yaliyolipwa na wakili kwa mchezaji filamu za utupu Stormy Daniels kabla ya uchaguzi wa 2016.
Hii ni mara yake ya kwanza kuzungumzia suala hilo. Alipoulizwa alipokuwa kwenye ndege ya Air Force One kama alifahamu kuhusu malipo hayo na fedha zilitoka wapi, Trump alisema "Hapana"
Alipoulizwa kwa nini wakili wake Michael Cohen alifanya malipo hayo, Trump alisema: "Inabidi umuulize Michael"
Muigizaji huyo anasema alifanya tendo la ndoa na Trump mwaka 2006. Trump amekana madai hayo.
Daniels, ambaye jina lake halisi ni Stephanie Clifford,anasema alisaini makubaliano ya kubaki kimya kuhusu uhusiano wake na Trump na kulipwa dola za Marekani 130,000 mwezi Oktoba 2016, kabla ya uchaguzi wa urais.
Daniels, ameviambia vyombo vya habari vya Marekani kuwa alitishiwa mwaka 2011 na mtu ambaye hakumfahamu aliyemtaka "kumwacha Trump"
Mawakili wa Trump wanataka kulipwa fidia ya $20m (£14m) na mwanamke huyo, wakisema alikiuka makubaliano ya kuweka siri ambayo aliyatia saini katika ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2016.
Mwanamke anayemtishia Donald Trum anasema madai hayo hayana msingi. Stephanie Clifford, alizaliwa Louisiana mwaka 1979.
Alihamia kwenye soko la kucheza filamu za utupu kwanza kama mtumbuizaji, kabla ya hapo mwaka 2004 alikuwa akiongoza na kuandika filamu.
Jina lake la jukwaani,Stormy Daniels, limetokana na jina la binti wa mwanamuziki wa kundi la Mötley Crüe, 'Storm' na jina la kinywaji aina ya Whisky , 'Jack Danniels'.
Unaweza kumtambua kwenye filamu ya 'The 40-Year-Old Virgin' na 'Knocked Up' na video ya muziki wa kundi la Maroon Five 'Wake up call' .
Mwaka 2010 alifikiria kugombea uongozi kwa nafasi ya useneti Louisiana lakini aliahirisha baada ya kusema kuwa ushiriki wake hautiliwi maanani.
Stephanie Clifford maarufu kama Daniels

No comments:

Post a Comment