Thursday, 26 April 2018

Sikwenda kumshawishi Trump na msimamo wake - Macron


Rais Emanuel Macron (kushoto) akipeana mikono na mwenzake Donald Trump
RAIS wa Ufaransa, Emmanuel Macron amemaliza ziara yake Marekani na kuonesha kuwa hajawa na ushawishi wa kutosha dhidi ya Rais Trump kubadili mtazamo wake kuhusu kujitoa katika mpango wa awali wa nyuklia dhidi ya Iran.
Trump anapinga makubaliano ya kimataifa yaliyofikiwa mwaka 2015, yanayolenga kuidhibiti Iran kuhusiana na mpango wake wa nyuklia.
Rais Trump anatarajiwa kuamua mwezi ujao iwapo atajitoa katika mpango huo. Hata hivyo, Macron katika mkutano wake na wanahabari amezungumzia suala hilo.
"Sina taarifa za ndani kuhusu uamuzi wa Rais Trump kuhusiana na mkataba wa nyuklia wa Iran (JCPOA). Kufuatia kile kinachodaiwa kwamba,nilimsikiliza alichosema kwamba inaonekana hana nia ya kuutetea mpango.
“Je nilichukulie suala hilo kama jambo binafsi?hapana,ninaamini hiyo ni makubaliano ya kampeni yaliyofikiwa kipindi kirefu kilichopita.Hivyo sijui nini itakuwa uamuzi wa Marekani katika suala hilo.
“Lakini ukiangalia mtazamo kuhusu suala hilo inaonekana hawezi kuunga mkono kuendelea na makubaliano ya JCPOA,” amesema Rais Macron
Macron amesisitiza kuwa hakuwa anajaribu kubadili msimamo wa Rais Trump kama atajitoa katika makubaliano, lakini badala yake atafanya kila linalowezekana kuhakikisha mpango wa nyuklia wa Iran unaendelea kuzuiwa.
"Wajibu wangu, hatua yangu,si kujaribu kumshawishi Trump, kujitenga na msimamo wake ama kubadilisha akili yake. Naamini tutakachokuwa tunakifanya ni kujenga mshikamano imara.
“Kwa hiyo jambo ninalolifanyia kazi ni kuhamasisha. Najaribu kuhakikisha mkataba huu unakuwa wenye tija, katika kukabiliana na kuthibiti shughuli za kinyukilia za Iran, na kuweka mikakati ya kidiplomasia ili kuhakikisha uamuzi wowote utakaochukuliwa na Rais Trump usituathiri.
“Hatuwezi kusema tutakosa upande iwapo Marekani itaamua kujitenga,'' amesisitiza
Kupitia ziara yake hii Rais Macron ameweza kuimarisha ushirikiano na Trump, japo katika maoni yake Macron anaonyesha kwamba si kwamba wamekubaliana kwa kila kitu yapo mambo ambayo wamekuwa na mtazamo tofauti.

No comments:

Post a Comment