Thursday, 12 April 2018

Sokoine ni mfano wa kuigwa na kila mtu – MagufuliRAIS Dk. John Magufuli amemwelezea Waziri Mkuu wa zamani, Hayati Edward Sokoine kuwa alikuwa msema kweli, asiyeogopa, mpiga vita rushwa, ufisadi, unyonyaji, mzalendo wa kweli na aliyechukia rasilimali za watanzania kuibwa na hivyo kuwa kielelezo cha ushujaa na mfano wa kuigwa na kila mtu.

Amesema yeye alimfahamu kiongozi huyo enzi za uhai wake kabla ya kufariki dunia tarehe kama ya leo ( April 12, 1984) ambapo Watanzania wanafanya kumbukizi ya kifo chake.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, Rais Magufuli ameandika Watanzania wanaadhimisha siku hiyo waige mfano wa Sokoine kwani alikuwa msema kweli.;

Katika siku kama ya leo tarehe 12 Aprili 1984 nikiwa Mpwapwa JKT nikitumikia jeshi langu “Oparesheni Nguvukazi” tukatangaziwa kifo cha marehemu Edward Moringe Sokoine, ilikuwa siku ya majonzi, shujaa huyu niliyemjua na kumshabikia ikawa siku yake ya mwisho.

Wakati tunapoazimisha siku kama hii ya kifo chake, watanzania tuige mfano wake kwani alikuwa msema kweli, asiyeogopa, mpiga vita rushwa,ufisadi, unyonyaji,mzalendo wa kweli na aliyechukia rasilimali za watanzania kuibwa.

Marehemu Sokoine hatasahaulika katika historia ya Tanzania, ni wito wangu kwa watanzania tumuige na kumuishi. Ni rai yangu pia tumuenzi kwa kujenga umoja wetu , kupiga vita rushwa na kuchapa kazi. Mungu aiweke roho ya marehemu Edward Moringe Sokoine mahala pema peponi.

Edward Moringe Sokoine aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyefariki dunia Aprili 12, 1984 kwa ajali ya gari, eneo la Dakawa nje kidogo ya mji wa Morogo.

No comments:

Post a Comment