Thursday, 12 April 2018

Spika aagiza Mayallah, wenzake kuhojiwa kwa madai ya kuandika habari kulichafua bungeJob Ndugai 

MWANAHABARI Paschal Mayallah na wahariri wa gazeti la wiki,  Raia Mwema wanatarajiwa kuhojiwa na Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge kwa madai ya kuchapisha habari inayodhalilisha Bunge, April 09, 2018.

Hatua hiyo imefikiwa mara baada ya mbunge wa Ulanga kupitia CCM, Goodluck Mlinga kuomba mwongozo wa Spika hapo juzi, April 09, 2018, akihoji iwapo habari iliyoandikwa na gazeti hilo yenye kichwa, 'Bunge linajipendekeza?' haidhalilishi Bunge.

Leo April 12, 2018 Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema habari hiyo ilidhamiria kuchafua hadhi ya Bunge na kueleza kuwa mwandishi huyo na wahariri watatakiwa kuhojiwa na kamati hiyo ya Bunge.

Utakumbuka Septemba 29, 27 gazeti hilo lilifungiwa kuchapishwa kwa kipindi cha miezi mitatu baada ya kuchapisha habari yenye kichwa ' Urais Utamshinda John Magufuli'.

No comments:

Post a Comment