Thursday, 12 April 2018

Spika atangaza utaratibu mpya wa namna ya kuingia bungeni


Job Ndugai


SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amelitangazia bunge leo kuhusu mabadiliko ya utaratibu wa kuingia bungeni.

Akifungua kikao cha bunge cha leo Aprili 12, Ndugai amesema utaratibu wa kuingia bungeni utabadilika ambapo  kuanzia sasa Spika, Naibu Spika na wenyeviti wa Bunge hawatatumia mlango mkuu kuingia ukumbi wa bunge,  bali mlango wa nyuma ila kwa matukio maalum.

“Utaratibu kama huo unatumika pia katika nchi nyingine kama India na Uingereza, nia ni kufanya maboresho kama mabunge yaliyoendelea,” amesema

Spika Ndugai amesema ingawa haimo kwenye kanuni, lakini mabadiliko hayo yanafanyika ili kuendana na nchi nyingine zilizoendelea.

No comments:

Post a Comment