Sunday, 22 April 2018

Takwimu za mimba Tabora zamtisha MwanriAggrey Mwanri

Mwandishi Wetu, Tabora

WATOTO wa kike 5913  wamepata ujauzito katika kipindi cha Januari hadi Machi mwaka huu, mkoani Tabora.

Mkuu wa mkoa huo, Aggrey Mwanri amebainisha hilo wakati akifungua semina ya siku moja ya kamati ya huduma za afya ya msingi ya mkoa huo.

Amesema takwimu hizo zinasikitisha na zinaoonesha kuwa bado kuna tatizo kubwa la watu wazima kukatisha ndoto za watoto wa kike mkoani humo.

Mwanri ameongeza kuwa halmashauri ya wilaya ya Nzega ndio inaoongoza kwa watoto 1438 , ikifuatiwa na Igunga 995, Kaliua ambayo ina watoto 894 , Sikonge 743, Uyui 640 , Urambo 630, Manispaa ya Tabora 530 na Nzega Mji 49.

Amesema vitendo hivyo sio vinarudisha nyuma maendeleo ya watoto bali vinawaweka katika hatari ya kupata saratani ya mlango wa kizazi kwa kushiriki ngono katika umri mdogo.

Mwanri amewaagiza viongozi na watendaji katika mkoa wa Tabora kuwafuatilia na kuwachukulia hatua haraka watu wote waliohusika na ujauzito wa watoto hao ili waweze kufikishwa katika vyombo vya sheria kujibu tuhuma zinazowakabili.

No comments:

Post a Comment