Saturday, 28 April 2018

Tatizo la nguvu za kike ni kubwa lakini halipo wazi


Mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai akizungumzia tatizo la wanawake wengi kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa.

Mwandishi Wetu

NI nadra kusikia watu wakizungumzia matatizo ya nguvu za kike, badala yake tumekuwa tukisikia matatizo ya nguvu za kiume.

Matatizo ya nguvu za kiume si tu yanazungumzwa na watu wa kawaida bali hata matabibu wa tiba za kizungu na wale wanaotumia mimea.

Wingi wa mabango yaliyotundikwa katika maeneo mbalimbali nchini, yanatia shaka kuwa huenda tatizo hilo ni kubwa kwa baba na kaka zetu hapa nchini.

Hakuna mabango yanayoonesha kutibu nguvu za kike na kama yapo basi ni machache hivyo kuifanya jamii ione kuwa tatizo hilo halipo kwa wanawake licha ya kwamba tunajua kuna ugumba na utasa.

Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai anasema wanawake wengi wanasumbuliwa na matatizo ya nguvu za kike.

Hata hivyo, anasema kutokana na tatizo hilo kuwa wazi zaidi kwa wanaume kwa maana ya maumbile yao, ni rahisi kujulikana huku wanawake wengi mno wakikabiliwa nalo lakini halijulikani.

Anabainisha kuwa halijulikani kwa sababu si rahisi kumgundua mwanamke mwenye tatizo hilo kwa kuwa mwenye anaweza kujifanya kama hana.

Ni pale anapokuwa na mwanaume anapoonesha kana kwamba ana hisia za kutaka kufanya tendo la ndoa huku uhalisia hajisikii chochote.

Mtaalam Mandai anasema tatizo hilo husababishwa na homoni za mwanamke kutokuwa za kawaida ama kuwa za juu zaidi ama chini.

"Kwa kawaida homoni za mwanamke inabidi ziwe 3269 au 8840, zikiwa chini ya hapo ama juu, mwanamke huyo anakuwa na tatizo la kutojisikia hamu ya kufanya tendo la ndoa, lakini anapokuwa na mwanaume anaweza kujionesha iwapo yupo tayari kwa tendo hilo mbele yake huku uhalisia anakuwa hana hisia yoyote," anasema.

Mtaalam huyo anasema kuwepo kwa kiwango cha chini cha homoni kunamfanya mwanamke akose hisia za kufanya tendo hilo licha ya kwamba anaweza kumwonesha mwanaume kama hana tatizo hilo.

Anatanabaisha kuwa licha ya kuwa hilo ni tatizo kubwa lakini wengi wao hukosa ujasiri wa kwenda kulitafutia ufumbuzi hospitalini au kwa matabibu wanaotibu kwa mimea na matunda.

"Ni vigumu wanawake kueleza matatizo yao ya kutojisikia hamu ya tendo la ndoa,"anasisitiza Mandai.

Hata hivyo, anasema wachache wenye ujasiri wa kwenda kwa matabibu wa tiba asili ama hospitali hukumbwa na changamoto ya kuwataka kimapenzi.

Anasema wanawashawishi kuwa iwapo watakubaliana watapona baada ya hapo.

Akimzungumzia mwanamke anayezaliwa akiwa na mayai na kwamba anapofikia umri wa miaka 9 hadi 12 homoni zake hupevuka mtaalam huyo anasema mwanawake mwenye tatizo hilo atumie mboga za majani kwa wingi pia ale tende, halua na asali.

Pia yeye anasema anazo dawa za mimea zinazosaidia kuamsha homoni za mwanamke na hivyo kumfanya kusika kuondokana na tatizo hilo na kufurahia tendo la ndoa.

"Uzuri wa dawa za asili zina uwezo wa kutibu magonjwa mengi tofauti na za kisasa. Mfano ukienda hospitali utapewa dawa ya metacafine kwa ajili ya kichwa tu, lakini dawa za asili dawa moja hutibu magonjwa mengi," anasema.

Kuhusu wanandoa ambao huishi pamoja muda mrefu bila kupata mtoto na wanapotengana kila mmoja wao huwa na mtoto anasema mmoja wao anakuwa na mbegu ama mayai ya moto na hivyo kushindikana kutungwa mimba.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho tiba vyetu.

No comments:

Post a Comment