Saturday, 14 April 2018

TBS, Star Media watiliana saini mkataba wa ushirikiano


Wawakilishi kwa upande wa serikali na wa Star Media katika picha ya pamoja.

Mwandishi Wetu Dodoma

KAMPUNI ya Star Media (T) Ltd yenye chapa ya StarTimes pamoja na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), zimetiliana saini Mkataba wa Makubaliano ya ushirikiano mjini Dodoma.

Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amesema mkataba huo utafungua ukurasa mpya wa manufaa kwa pande zote mbili.

“Kama alivyosema Waziri Mkuu nina matumaini makubwa sana na ushirikiano huu, kwa sababu kupitia ushirikiano huu ndio tutaona TBC ikipanda kiteknolojia, ikipanda kivifaa na ikipanda kwa weledi”, amesema Dk. Mwakyembe.

Akizungumzia kwa upande wa wizara na nafasi yake amesema, “Ni wajibu wa wizara kuhakikisha yote tuliyokubaliana yanatekelezwa. 

Akizungumzia mkataba huo Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Dk. Ayoub Rioba amesema kasoro zilizokuwepo awali sasa zimeondolewa ili kuanza ukurasa mpya na yeye kwa upande wake atakuwa Mwenyekiti wa Bodi huku TBC ikimiliki asilimia 35. 

“Makubaliano haya ambayo tumesainiana leo (jana)ni kuondoka kule ambako tumekuwa twende katika muktadha mpya, ambapo kampuni itaendeshwa kwa uangalizi wa karibu sana, watanzania na mimi kama mwenyekiti wa bodi tumeshaanza kuanzia hivi ninavyozungumza kuna namna tunafanya mambo tofauti ili tuhakikishe tunasimamia vizuri hiyo mampuni”.

Rioba pia alizungumzia upiaji upya wa mikataba ili kuondoa kasoro za awali anasema; “Moja ya makubaliano ni kwamba tutapitia upya mkataba na tumeshaanza,  wao wameshaona mambo ambayo yana kasoro kwa upande wao sisi pia tumeona kwa upande wetu na wote tumeyajadili tumeona kuna kukubaliana kwa hiyo kinachofuata tunaangalia upya ule mkataba wa Ubia ili zile kasoro nyingine za msingi ambazo zilisababisha uendeshaji kutokuwa mzuri tunaziondoa ili tuende katika namna ambayo hatutarudia tena kuwa na matatizo ambayo tumekuwa nayo.

No comments:

Post a Comment