Wednesday, 11 April 2018

Tehama itumike kulinda mabadiliko ya tabia nchi – Prof MbarawaWaziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo wakati akifungua Mkutano wa Nane wa Wiki ya Kijani wa Shirika la Mawasiliano Duniani (Itu), unaohusu namna ya kutumia Tehama kuendana na mabadiliko ya tabianchi unaofanyika Zanzibar.Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Viwango wa Shirika la Mawasiliano Duniani (Itu) Dk. Chauseb Lee kuhusu ushirikiano baina ya Tanzania na Itu namna ya kutumia Tehama kuendana na mabadiliko ya tabia nchi wakati wa Mkutano wa Nane wa Wiki ya Kijani unaofanyika Zanzibar.Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi James Kilaba (katikati) akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wakati wa mkutano wa Nane wa Wiki ya Kijani wa Shirika la Mawasiliano Duniani (Itu)  uliofanyika Zanzibar kuhusu namna ya kutumia Tehama kuendana na mabadiliko ya tabianchi. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Mawasiliano wa wizara hiyo, Mhandisi Maria Sasabo.Mkurugenzi wa Shirika la Mawasiliano na Viwango Duniani (Itu), Dk. Chauseb Lee akifafanua jambo kwa wadau wa Tehama wakati wa mkutano wa Nane wa Kijani kuhusu namna ya kutumia Teknolojia hiyo kuendana na mabadiliko ya tabianchi unaofanyika Zanzibar.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (aliyeketi katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa Tehama kwenye mkutano wa Nane wa Wiki ya Kijani wa Shirika la Mawasiliano Duniani (Itu), unaohusu namna bora ya kutumia Tehama kuendana na mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika Zanzibar.
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Sira Ubwa Mwamboya akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Mhandisi, James Kilaba wakati wa Mkutano wa Nane wa Wiki ya Kijani wa Shirika la Mawasiliano Duniani (Itu), pamoja na mambo mengine ulioadili kuhusu namna bora ya kutumia Tehama kuendana na mabadiliko ya tabianchi uliofanyika Zanzibar. Katikati ni Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi Peter Ulanga.


Prisca Ulomi, WUUMWADAU wa Shirika la Mawasiliano Duniani (Itu), wanaohusika na masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), wanakutana hapa nchini kwenye Mkutano wao wa Nane.

Washiriki hao kutoka nchi mbali mbali duniani, wanakutana katika Wiki ya Kijani ili  kujadiliana namna ya kutumia Tehama kuendana na mabadiliko ya tabianchi yanaoendelea kutokea duniani.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amefungua mkutano huo unaofanyika Zanzibar ambao umeandaliwa na wenyeji Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Akifungua mkutano huo, Prof. Mbarawa amewataka wataalamu wote wa Tehama kutoka sehemu mbali mbali duniani, kutumia mkutano huo kujadiliana, kuweka mikakati na miongozo ya namna ya kutumia huduma na bidhaa za Tehama kwa maendeleo ya uchumi wa viwanda ikiwa ni pamoja na mbinu za kutabiri na kudhibiti majanga yanayotokea kuendana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kutumia teknolojia hiyo.

Amewataka washiriki wa mkutano huo kubadilishana uzoefu na kujadiliana namna ya kutumia Tehama kulinda mazingira, kufungua fursa za kiuchumi, kuwa na miji ya kisasa ambayo inaendeshwa na kusimamiwa kwa kutumia teknolojia hiyo ili kuhakikisha kuwa  inatumika kutunza na kulinda mazingira ili kupunguza uchafuzi wake.

Amefafanua kuwa Tanzania imejenga mkongo wa taifa wa mawasiliano wenye urefu wa zaidi ya kilomita 25,000 ambao umeunganishwa kwenye taasisi za Serikali na sekta binafsi na kwenye nchi jirani ambazo hazijapakani na bahari ambapo umewezesha utoaji wa huduma za mawasiliano nchini ambapo hadi hivi sasa tuna watanzania milioni 45 wanaotumia simu za mkononi, milioni 23 wanaopata huduma za intaneti na milioni 20 wanaotumia huduma za kielektoniki kama vile kutuma na kupokea fedha.

Naye Mkurugenzi wa Itu, Dk. Chaesub Lee amewataka wataalamu hao kujadiliana na kupeana uzoefu kutoka kwenye nchi zao na kutumia fursa za Tehama kuongeza mzunguko wa uchumi wa viwanda duniani, kutumia bidhaa na huduma za teknolojia hiyo kulinda mazingira na kuchakata bidhaa na huduma za mawasiliano ambazo zimepitwa muda wake au kuharibika.

Amesema Itu iko tayari kushirikiana na nchi husika katika nyanja ya utalaamu, ushauri na utekelezaji wa mipango na mikakati mbalimbali ya namna ya kutumia Tehama kuendana na mabadiliko ya tabianchi kulingana na mahitaji ya nchi husika.

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Sira Ubwa Mwamboya wakati akifunga mkutano huo, amewakaribisha washiriki hao kutembelea vivutio mbali mbali vya kiutalii vilivyopo kwenye visiwa hivyo.

No comments:

Post a Comment