Wednesday, 25 April 2018

Tumemwandikia barua IGP tishio la kuuawa kiongozi wetu - Shaibu

CHAMA cha ACT Wazalendo kimesema kimetuma barua kwa IGP kumpa taarifa za tishio la kuuawa kwa Kiongozi wao, Zitto Kabwe.

Akizungumza na wanahabari jana kwenye ofisi za chama hicho Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi, Mawasiliano kwa Umma na Uenezi, Ado Shaibu amesema wao wamepokea taarifa hizo kutoka kwenye mitandao ya kijamii.

Katibu huyo ameongeza kuwa hawawezi kupuuzia taarifa hizo kwa kuwa hadi jana bado haifahamiki Ben Saanane yuko wapi.

Ado Shaibu 

“Lakini tumemwandikia barua IGP ili achunguze taarifa hizo, hatuwezi kupuuza kwa sababu Chadema ililalamika kabla ya shambulio la Tundu Lissu, hatupuuzi kwa sababu, leo hii hatujui Ben Saanane yuko wapi,” amesema katibu huyo.

No comments:

Post a Comment