Saturday, 7 April 2018

Tumia karoti kulainisha uso, matatizo ya koo na vidonda vya tumbo


Rangi mbalimbali za karoti

KAROTI ni kiungo katika vyakula vya aina mbalimbali zikiwemo mboga ambacho kinachochea radha nzuri katika vyakula.

Asili ya karoti ni Persia huko Ulaya na Kusini Magharibi mwa Asia. Kwa Tanzania zao hili hulimwa hasa mikoa ya Iringa, Mbeya, Morogoro, Arusha, Kagera na Kilimanjaro.

Kwa kawaida karoti huwa na rangi ya machungwa, zambarau, nyeusi, nyekundu, nyeupe na njano. Karoti za sasa zimetokeza kutokana na karoti pori, (Daucus carota).

Karoti pia hutumika kwenye kachumbari na pia zinafaida kubwa katika mwili kwa kuupatia vitamin A na C pamoja na madini ya chuma.

Kiungo hiki kinafaida nyingi ikiwemo wingi wa vitamini, inapigana na kusaidia katika maradhi ya upungufu wa damu, kulainisha tumbo pamoja na uvimbe wa saratani.

Pia inasafisha damu, kuondoa chunusi, tatizo la vidonda vya tumbo, matatizo ya koo na kibofu.

Chukua karoti kilo moja, ponda laini weka maji lita mbili, chemsha kwa muda wa dakika 15, tumia kikombe kimoja kutwa mara tatu, juisi yake pia hulainisha uso.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment