Saturday, 14 April 2018

Tumia mchaimchai una faida nyingi kwa afya yako


Mchaichai

MCHAICHAI ni moja ya mazao yanastawishwa hapa nchini. Wakulima wanalima zao hilo kwa ajili ya kujipatia fedha lakini ni pia wanalitumia wao na jamaa zao kwa kuwa ni kinywaji chenye radha na harufu nzuri.

Hata hivyo, mchaichai una faida nyingi nyingine ambapo wenye magonjwa ya shinikizo la damu, unasaidia kusafisha figo, maumivu ya tumbo wakati wa hedhi na kinga dhidi ya aina mbalimbali za maradhi ya saratani.

Hilo limebainika kutokana na tafiti mbalimbali zilizobaini uwezo mkubwa wa mchaichai hata katika umenyenyaji wa chakula tumboni.

Kutumia mchaichai, weka majani yake ndani ya maji yanayochemka, chemsha kwa muda wa dakika 15, kunywa kikombe kimoja na nusu cha chai kutwa mara tatu.

Aidha, unapokumbwa na tatizo linalohitaji kutumia mchaichai ni vema uje makao yetu makuu ambapo utapata maelezo ya kina ya namna ya kutumia mmea huu na faida zake nyingi nyingine.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment