Sunday, 8 April 2018

Tumia mchicha kwa tatizo la tezi la shingo


Mchicha

MCHICHA ni moja ya mboga za majani maarufu sana katika ukanda wa Afrika Mashariki. Pamoja na faida nyingine kula mchicha kunaondoa tatizo la uoni hafifu.

Mchicha ambao wastawishaji wamekuwa wakinufaika kwa kupata fedha nyingi kwa muda mfupi, pia unasaidia kwa wenye matatizo ya maumivu ya mgongo, unasafisha njia ya mkojo, unasafisha damu, unasaidia kwa wenye matatizo ya figo, unasadia kupata haja ndogo kwa wingi, unasaidia kwa mwenye matatizo ya kuhara damu na minyoo.

Kalikadhalika, unasaidi kwa anayesumbuliwa na homa inayotokana na mafua, unaongeza damu, lakini pia ni dawa ya wale vikojozi.

Unapotumia mchicha kwa kuondoa matatizo mbalimbali unapaswa kuchukua kilo moja ya majani ya mchicha, kisha chemsha maji lita mbili na nusu, uloweke ndani ya maji hayo kwa muda wa dakika 15. Tumia kikombe kimoja cha chai. Ni vema ukatumia maji yote kwa muda wa siku moja.

Mwenye tatizo la tezi la shingo achukue mchicha kidogo, auponde kisha aufunge shingoni pale kwenye uvimbe wakati anapolala kwa muda wa siku tano (kila siku atoe na kuweka mwingine).

Anayesumbuliwa na maumivu ya mgongo, usiku wakati wa kulala anashauriwa kupasha moto mchicha kisha aufunge mahali anaposikia maumivu alale nao, ili vuguvugu la joto lenye maji ndani liingie. Afanye hivyo kwa muda wa siku tano huku akiweka mpya (mwingine) kila siku.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au awasiliane na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment