Wednesday, 11 April 2018

Tumia stafeli ni kinga na msaada wa maradhi tishioTunda la Stafeli


STAFELI ni tunda ambalo limebainika kuwa na uwezo mkubwa wa kusaidia maradhi mbalimbali zikiwemo aina za saratani.

Asili ya stafeli ni Amerika Kusini, licha ya kuwa sasa linastawishwa katika maeneo mbalimbali duniani ikiwemo hapa nchini.

Linastawi katika maeneo yenye miinuko, huku tafiti zikibaini uwezo mkubwa wa tunda hilo kusaidia matatizo mbalimbali ya kiafya bila shaka pamoja na mambo mengine ni wingi wa nyuzinyuzi (fible), zilizolisheheni.

Stefeli lina uwezo mkubwa wa kusaidia na kuzuia maradhi mbalimbali hivyo ni vema jamii iamke ianze kujenga utamaduni wa kulitumia tunda hilo mara nyingi itakavyoweza.

Licha ya tafiti kuonesha kuwa stafeli lina uwezo wa kukinga dhidi ya aina mbalimbali za saratani kama ya titi, kibofu cha mkojo,  ya shingo ya kizazi, pia linasaidia matatizo ya vidonda vya tumbo.

Tafiti zimeonesha kuwa stafeli lina uwezo wa kudhibiti madhara ya saratani bila kuleta athari katika mwili wa mgonjwa tofauti na ilivyo kwa tiba za kisasa zikiwemo zile za mionzi.

Ni vema jamii itumie stafeli japo kwa wiki mara tatu ili kujikinga na maradhi mbalimbali ambayo yamekuwa tishio nyakati hizi za utandawazi. Unaweza kula tunda lenyewe, au kutumia juisi yake.

Majani ya tunda hilo yakitumika kitaalamu yanasaidia kuzuia matatizo ya uvimbe katika kizazi kwa wanawake.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho vyetu.

No comments:

Post a Comment