Thursday, 5 April 2018

Tumia tango linasaidia kupambana na maradhi mengi


Tango
MIONGONI mwa matunda ambayo ni muhimu kula ili kuukinga mwili dhidi ya maradhi mbalimbali ni pamoja na tango.

Tango moja lina vitamin B1, B2, B3, B4 na B6, madini ya chuma, potasium na zinc. Pamoja na kuukinga mwili na maradhi unapojisikia umechoka mchana, kula tango moja linaweza kukupa nguvu kwa muda wa saa kadhaa.

Tunda hilo  asili yake katika bara la Asia, hasa nchini India. Unaweza kulitumia kwa kulitafuna baada ya kuosha kwa maji safi na salama au kunywa juisi yake baada ya kuitengeneza.

Ikiwa unasumbuliwa na magonjwa ya saratani, vidonda vya tumbo na ngozi tumia tango mara kwa mara utaona matokeo bora kwa kuwa pamoja na mambo mengine lina nguvu kubwa ya kuondoa uriki asidi mwilini.

Tango linasafisha utumbo mwembamba na kutibu tumbo kwa ujumla. Tunda hili linaondoa au kuzuia ugonjwa wa ini, figo na koo. Juisi ya tango inasaidia mwili kufanya kazi vizuri.

Vitamini na madini mengi yapo kwenye ganda la tango, hivyo unapolitumia usitoe maganda licha ya kuwa mengine ni machungu lakini hufaa zaidi.

Watu walio na mikono yenye michubuko na iliyokauka watumie kupaka au kujipaka mwili mzima. Weka katika beseni juisi ya tango, tumia kuosha uso au mwili. Matumizi ya tango kama chakula huondoa sumu zinazotokana na kemikali.

Tango linaondoa chunusi, majipu na michaniko mwilini pia baridi yabisi, kuvimba miguu na linaondoa uriki asidi mwilini.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho vyetu.


No comments:

Post a Comment