Tuesday, 24 April 2018

Ulaji kwa wingi vyakula vyenye madini ya phosphorus husababisha figo


Mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai akizungumzia umuhimu wa jamii kula kwa kiasi vyakula vyenye madini ya phosphorus kuepuka maradhi ya figo.KUKUA kwa utandawazi duniani kumeleta faida na hasara pia kwani wakati faida ikiwa ni pamoja na dunia kuwa kama kijiji kupitia mawasiliano ya mitandao, magonjwa mbalimbali nayo yameshika kasi tofauti na ilivyokuwa hapo zamani kabla ya utandawazi.Uzoefu unaonesha kuwa kabla ya utandawazi moja ya magonjwa yaliyokuwa yakiitafuna jamii ya Kitanzania ulikuwa ni pamoja na homa ya manjano ambayo ilikuwa kikwazo cha maendeleo lakini kwa sasa hali imezidi.

Zipo simulizi kuwa kabla ya kuenea zaidi kwa utandawazi, baadhi ya magonjwa kama figo na kisukari yalikuwa ni nadra kuwapata watu wengi zaidi kama ilivyo sasa.

Magonjwa hayo yasiyoambukiza yanatokana na ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi lakini pia wanajamii kutofanya mazoezi ya viungo.

Simulizi hizo zinabainisha kuwa aina ya vyakula vya asili vilivyokuwa vikitumiwa na Watanzania kabla ya utandawazi vilikuwa kichocheo cha kuwakinga na magonjwa mbalimbali ambayo kwa sasa  yameshika kasi.

Pia walikuwa wakifanya kazi nyingi za kutumia nguvu kama sehemu ya mazaoezi tofauti na sasa watu wanafanya kazi ambazo hawatumii nguvu sanjari na kutumia usafiri hata kama wanakwenda eneo jirani ukilinganisha na zamani walikuwa wakitembea umbali mrefu kwa miguu ambapo ilikuwa sehemu ya mazoezi tosha.

Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai anasema ugonjwa sugu wa figo ni miongoni mwa maradhi maarufu zaidi miongoni mwa watu wenye umri mkubwa wa kuanzia miaka 60 na kuendelea.

Anasema ugonjwa huo ni moja ya matatizo ya kiafya yanayojitokeza kuchukua chati kubwa  miongoni mwa magonjwa ambayo yanawasumbua wengi kwa sasa hapa nchini.

Mandai anabainisha mambo kadhaa yanayohusishwa na ongezeko la ugonjwa sugu wa figo kuwa ni pamoja na ugonjwa wa kisukari, shinikizo la damu, unene kupita kawaida na uzee.

Pia mabadiliko katika tabia na namna watu wanavyoishi navyo vimeonekana kuchangia ongezeko la ugonjwa huo kwa kiasi kikubwa.

Anatanabaisha mtaalamu huyo kuwa licha ya kwamba ugonjwa sugu wa figo hutokana na magonjwa kadhaa ambayo kimsingi yanaathiri figo yenyewe, visababishi vikuu vya ugonjwa sugu wa figo ni kisukari na shinikizo la damu.

Mandai anasema matumizi ya muda mrefu ya baadhi ya dawa za kutuliza maumivu kama vile brufen au acetaminophen zinaweza pia kusababisha ugonjwa huo.

Mtaalamu huyo anasema matumizi ya baadhi ya dawa kama gentamicin pia husababisha madhara katika figo na hatimaye kusababisha ugonjwa sugu wa figo.

Pia anasema hali ya mishipa ya damu inayosambaa kwenye figo inapozeeka hupungua kipenyo chake na kuwa migumu kiasi cha kushindwa kutanuka na kusinyaa vema ambapo husababisha upungufu mkubwa wa damu katika figo husika kwa kitaalam hujulikana kama ischemic nephropathy.

Aidha, Mandai anasema mtu anaweza kuepuka kupata ugonjwa sugu wa figo kwa kupunguza kiwango cha protini anachokula ambapo hupunguza kasi ya kuharibiwa kwa figo.

Pia ni vema matumizi ya chumvi katika chakula yakapungua ili kuepusha mrundikano wa maji mwilini na kusaidia kuthibiti shinikizo la damu.

"Kiasi cha chumvi kinachoshauriwa ni kati ya gramu nne hadi sita kwa siku," anasema.

Anaongeza kuwa jamii inapaswa kupunguza au kuepuka vyakula vyote vyenye madini ya potassium kwa wingi.

"Kupunguza vyakula vyenye madini ya phosphorus kama vile mayai, maharagwe, vinywaji vyote vya jamii ya cola, mazao yote ya maziwa, mtindi, jibini, siagi na jamii zake, husaidia kuilinda mifupa isizidi kuathirika," anasema.

Mtaalamu huyo anawaonya wavuta sigara kuachana na uvutaji kwani moja ya athari wanazoweza kupata ni pamoja na ugonjwa sugu wa figo.

"Kama mnene jitahidi kupunguza uzito kwa kadili utakavyoshauriwa na daktari, pia epuka kutumia dawa yoyote bila kushauriwa na daktari," anasema.

Licha ya ugonjwa huo kuwa tishio, Mandai anasema ipo mimea tiba inasaidia kukabili ugonjwa huo.

Anasema mimea tiba ina uwezo wa kudhibiti kiwango cha sukari na shinikizo la damu lakini pia mrundikano wa maji mwilini kwa kutumia dawa ya kutoa maji.

Mtaalam huyo anafafanua kuwa mimea tiba inaweza kumfanya mgonjwa kupunguza na kutoa nje madini ya phosphorus na kuongeza vitamini D.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho vinavyozalishwa na kampuni yetu.

No comments:

Post a Comment