Tuesday, 24 April 2018

Unataka kuacha ulevi? Tumieni kabichi


Mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai akizungumzia umuhimu wa kabichi ambayo hutumiwa na jamii kama mboga, lakini pia inasaidia kukabiliana na changamoto za kiafya.KABICHI ni aina ya mboga inayopatikana kwenye maeneo mengi Ulimwenguni licha ya kuwa inatofautiana rangi kulingana na eneo inakostawishwa.

Wakati jamii kubwa ikiitegemea kuitumia kabichi kama mboga, wataalam wanatoa tiba kwa kutumia mimea wanasema ni dawa nzuri inayosaidia kukabiliana na changamoto za maradhi zinazo ikabili jamii.

Kuna ugumu kidogo kuelezea historia ya Kabichi, lakini ni zao ambalo liligunduliwa na lilikuwa likitumika Ulaya miaka 1000 BC.

Hapa nchini kabichi inastawishwa zaidi katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Morogoro, Tanga, Iringa na Mbeya. Kabichi ina madini aina ya chokaa, kambakamba, protini na maji kwa wingi.

Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai anasema mboga hiyo wengi huitumia katika maisha ya kila siku huku wakiwa hawana uelewa nayo iwapo inasaidia kukabiliana na changamoto za kiafya.

Mandai anasema kabichi ikitumika vizuri inaweza kusaidia kuondokana na matatizo ya kikohozi sugu pamoja na wale wenye matatizo ya usagaji wa chakula tumboni.

Anafafanua faida nyingine ya kabichi ni kuondoa minyoo, pumu, pamoja na chunjua, hali kadhalika huweza kutumika kama kisafisha tumbo kwa kumsaidia mtu kuhamasisha kuharisha.

Anasema mboga hiyo huwasaidia wale wenye matatizo ya pumu na inapunguza unene, lakini pia ni kibandiko kinachomsaidia mwenye kidonda, uvimbe na sehemu yenye maumivu.

Hata hivyo, kabichi ina rangi tofauti, miongoni mwazo ni kijani ambayo tumeizoea na zambarau. 
 
Ajabu nyingine ya kabichi ni kwamba ina uwezo wa kumfanya mtumia kilevi hususan pombe lakini anashindwa kuiacha, kuachana nayo kabisa.

"Kabichi inaweza kuvunja tabia ya kuzoea ulevi, ili kufanikisha hilo mhusika anapaswa kunywa juisi ya kabichi kwa kutumia kijiko kimoja kikubwa kila saa.

"Mtumiaji wa mboga hii daima hubaki katika mwonekano mzuri hasa katika masuala ya utunzaji wa nywele. Kwenye nywele mtumiaji anashauriwa kuzioshea kwa juisi mara mbili kutwa,"anasema mtaalam huyo.

Pamoja na hayo pia kabichi huondoa vijipele vinavyojitokeza juu ya ngozi na pia inatibu vidonda vya tumbo.

Licha ya faida lukuki za kabichi, Mandai anawaonya watumiaji kuitumia kwa kiasi kwa kuwa matumizi kupita si mazuri yanahamasisha shida ya koo na kusababisha goita.

Anatoa mwito kwa watumiaji kutotumia aina yoyote ya dawa bila kumwona mtaalam wa masuala ya afya ili kumpa maelekezo stahiki kuhusu dawa husika anayotaka kuitumia.

Mtaalam huyo anayehamasisha ulaji wa mboga na matunda kwa wingi, anawataka wanajamii kustawisha au kununua vyakula hivyo kwa wingi ili kuzingatia mlo mchanganyiko unaosaidia kulinda afya ya mlaji.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho vinavyozalishwa na kampuni yetu.

No comments:

Post a Comment